Kanali ya Kizayuni: Israel inakabiliwa na Intifadha mpya ya Wapalestina

Chombo kimoja cha habari cha Kizayuni kimesema hali ya usalama katika eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan linalokaliwa kwa mabavu ni ya ‘hatari’ na kwamba Tel Aviv inakabiliwa na Intifadha mpya ya Wapalestina.

Kwa mujibu wa mwandishi wa habari wa Kanali ya 12 ya Kizayuni, tangu kuanza kwa operesheni za hivi karibuni katika Ukanda wa Gaza, Israel imevimimina vikosi vyake vamizi katika eneo hilo linalokaliwa kwa mabavu la Wapalestina.

Taarifa hiyo imethibitishwa na mchambuzi wa masuala ya kijeshi wa Kizayuni, Amir Bar Shalom ambaye anasema: Hali ya usalama katika eneo la Ukingo wa Magharibi inaonesha wazi hatari inayotukabili, nayo ni Intifadha ya Pili.

Amesema wimbi la hivi sasa la mashambulizi ya Wapalestina lililoanza tangu Machi mwaka huu katika Ukingo wa Magharibi linatazamiwa kupanuka zaidi katika siku zijazo.

Shalom amesema tayari jeshi la Israel limeshapiga kengele ya hatari, na kusisitiza kuwa Intifadha mpya ya Wapalestina huenda ikatokea ndani ya miezi michache ijayo, na wala si baada ya miaka kadhaa kama ilivyokisiwa hapo awali.

Harakati na makundi yote ya muqawama yametangaza kuunga mkono Intifadha na mwamko wa wakazi wa Ufukwe wa Magharibi wa Mto Jordan dhidi ya Wazayuni maghasibu.

Si vibaya kuashiria hapa kuwa, Intifadha ya al-Aqsa ilianza tarehe Mosi Oktoba 2000 na kuendelea hadi tarehe 8 Februari 2005 wakati kulipotiwa saini hati ya usitishaji vita huko Sharm Sheikh nchini Misri.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *