Kan’ani: Jeshi la SEPAH ni chombo muhimu mno cha kupambana na ugaidi duniani

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiisamu ya Iran amejibu hatua ya Bunge la Ulaya iliyo dhidi ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH na kusisitiza kuwa, SEPAH ni chombo kikubwa na muhimu zaidi cha kupambana na ugaidi duniani.

Matamshi hayo ya Nasser Kan’ani yametolewa baada ya Bunge la Ulaya kupigia kura ya ndio kipengee cha kulitambua jeshi la SEPAH la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuwa eti ni katika makundi ya kigaidi.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amenukuliwa na shirika la habari la Iran Press akisema hayo na kuongeza kuwa, utawala wa kimla na wa ubaguzi wa rangi wa Israel ndiye gaidi mkubwa wa kitaasisi duniani, tawala za kiistikbari na kibeberu za Marekani na Uingereza ndizo zilizolianzisha na ndio waungaji mkono wakuu wa donda-ndugu hilo la kensa yaani Israel katika eneo la Asia Magharibi.

Aidha amesema, sababu iliyoyafanya madola ya kibeberu yanayoeneza vitendo vya kigaidi duniani, kuhamakishwa na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH ni kutokana na kuwa jeshi hilo ndiye mpambanaji mkubwa zaidi wa vitendo vya kigaidi duniani na hilo haliyafurahishi madola ya kiistikbari ambayo ndio waungaji mkono wakuu wa ugaidi ulimwenguni.

Kabla ya hapo pia Mohammad Bagher Ghalibaf, Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) alikuwa amesema kwamba, kitendo cha kiwoga cha Bunge la Ulaya cha kuliweka jeshi la SEPAH katika orodha ya kile kinachodaiwa ni makundi ya kigaidi, hakitoachwa vivi hivi bila ya kupata majibu makali kutoka kwa Jamhuri ya Kiislamu.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *