Katika kivuli cha mwendelezo wa kuzingirwa, watoto wa Yemen wanakufa

Ripota wa habari nchini Yemen aliripoti kuhusu hali mbaya ya watoto nchini humo kutokana na miaka ya vita na mzingiro.

Udhaifu wa mwili na hali ya kukond ilidhihirika usoni mwa kijana Taysir kutoka Yemen, kijana huyo mwenye umri wa miaka kumi na tatu alikua na uzito wa kilo tano. Na hali hii imemfanya ashindwe kutembea sawa kama watoto wengine wa rika lake, hana uwezo wa kupumua kwa urahisi, na anasubiri yupo ni kana kwamba anasubiri kifo kitandani.

Umaskini uliokithiri na utapiamlo unaosababishwa na kuzingirwa kwa Yemen umesababisha idadi ya watoto walio chini ya umri wa miaka mitano kukabiliwa na ugonjwa wa utapiamlo na visa vyake kuongezeka nchini humo.

Hii ni licha ya kuwa vituo vya matibabu vinakosa uwezo wa kuwatibu watu hao kutokana na kusitishwa kwa misaada kutoka kwa mashirika ya kimataifa na ukosefu wa usalama wa chakula.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *