Kenya yasema Wanajeshi wa Afrika Mashariki nchini DRC ‘walifanikiwa’

Serikali ya Kenya imesisitiza kuwa Jeshi la Kikanda la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EACRF) lililohudumu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) hadi Desemba mwaka jana lilikuwa na mafanikio makubwa.

Katika hotuba mjini Nairobi, Waziri Kiongozi wa Kenya ambaye pia Waziri wa Masuala ya Kigeni Musalia Mudavadi alitetea jeshi hilo la kikanda ambalo limelaumiwa kwa kushindwa kusambaratisha  makundi yenye silaha, akisema jeshi hilo lilikuwa nalengo tu la kudumisha amani.

Jeshi la Kikanda la Jumuiya ya Afrika Mashariki ilitumwa DRC mnamo Novemba 2022 kwa miezi sita ya awali, ambayo iliongezwa hadi Desemba mwaka jana.

Askari hao wa Afrika Mashariki waliondoka DRC kufuatia  malalamiko ya serikali ya nchi hiyo ambayo, ilidai askari hao wa kikanda walishindwa kulenga kundi la waasi la M23 linalochukuliwa kuwa tishio kubwa kwa DRC mashariki mwa Kongo.

Kufuatia kutumuliwa askari hao wa Afrika Mashariki, serikali ya DRC imegeukia Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), ambayo tayari imepeleka wanajeshi 5,000 mashariki mwa nchi hiyo.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *