Khatibu wa Msikiti wa al-Aqswa aonya kuhusiana na njama za Israel za kuiyahudisha Quds

Khatibu wa Msikiti wa al-Aqswa huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu ameonya kuhusiana na njama za jeshi vamizi la Israel la kuuyahudisha mji wa Quds na kuudhibiti mji huo.

Samahat Sheikh Ekrima Sabri Khatibu wa Msikiti wa al-Aqswa ametahadharisha piia kuhusiana na njama za kila leo za utawala vamizi wa Israel kuugawa msikiti wa al-Aqswa kiwakati na kieneo.

Khatibu wa Msikiti wa al-Aqswa amebainisha kuwa, hivi karibuni tumeshuhudia uvamizi mtawalia wa Wazayuni unaofanyika kwa sura jumla tena kwa kuungwa mkono na wanajeshi wa utawala vamizi wa Israel.

Mwanazuoni huyo ameongeza kuwa, ufahamu wa hali ya juu wa wakazi wa mji mtakatifu wa Quds ni kizingiti imara mkabala wa njama zote haribifu za wavamizi ambazo zina lengo la kuwapiigisha magoto na kuwafanyua Wapalestina wasalimu amri na hivyo kuidhibiti Quds.

Sheikh Sabri amewahi kukamatwa mara kadhaa na wanajeshi wa Israel kwa visingizio mbali mbali kama vile kuunga mkono mapambano ya ukombozi wa Palestina na kupinga wazi hatua ya baadhi ya nchi za Kiarabu ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Utawala wa Kizayuni unatekeleza misingi mitatu mikuu ambayo ni kuugawa utumiaji wa Msikiti wa Al Aqsa kisehemu na kiwakati, kuchimba mashimo ya chini kwa chini na kandokando ya msikiti na kuyahudisha maeneo ya jirani na mahala hapo patakatifu.

Hii ni katika hali ambayo, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limethibitisha tena kwamba msikiti mtukufu wa Al-Aqsa, kibla cha kwanza cha Waislamu ni milki ya Wapalestina.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *