Kifo cha Malkia na Uhalifu wa Uingereza

Kifo cha Malkia na Uhalifu wa Uingereza

Na Ustad Syed Jawad Naqvi

 

Malkia hastahili maombolezo na huzuni kutoka kwa mataifa ya Kiislamu

Alikuwa na umri wa miaka 96 alipofariki na alibaki madarakani kwa miaka 70 . Kwa mujibu wa habari Uingereza na nchi zote za jumuiya ya madola chini ya Uingereza ikiwa ni pamoja na Pakistan zimetangaza huzuni na maombolezo asubuhi ya leo.

Alikuwa mkuu wa Uingereza pamoja na wanachama wa nchi za Jumuiya ya Madola miongoni mwao nchi ya Pakistan. Nchi za Jumuiya ya Madola kwa maelezo rahisi ni hizi nchi zinazocheza mchezo wa kriketi na kiukweli ni zile nchi zilizobaki kuwa chini ya ukoloni wa utawala wa Waingereza na familia ya malkia ilitawala nchi hizi.

Hadi sasa karibu nchi 14 bado ni makoloni ya Uingereza ambayo inajumuisha baadhi ya visiwa. Baadhi ya nchi kubwa kama vile Australia, New Zealand, Kanada zinatawaliwa rasmi na Uingereza na visiwa vyengine vipo chini ya utumwa wa Uingereza.

Lakini baadhi ya nchi kama vile Pakistani ambazo licha ya kupata uhuru bado zimejitolea kubaki watumwa wa Uingereza kwa hiari. Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Madola wametoa rambirambi zao na kutangaza maombolezo.

Rais na waziri mkuu wa Pakistani wote wamewasilisha rambirambi kutoka ndani ya mioyo yao na pia kutangaza kipindi cha huzuni na maombolezo. Wamesema kuwa taifa zima (la Pakistani) liko chini ya majonzi ya kifo chake.Vile vile inapaswa kutokea wakati chifu wa taifa anapofariki iwe siku ya majonzi ya asili kwa watu wa taifa hilo lakini kwa baadhi ya nchi kama Pakistan kuwa na huzuni kwa kifo cha malkia haikubaliki kimantiki..

Ingawa baadhi ya nchi kama vile Argentina zinasherehekea hadharani kifo chake pasi na kuwepo kwa tangazo rasmi kutoka kwa serikali. Hii ni kwa sababu sote tunajua uhusiano kati ya Argentina na Uingereza, kumekuwa na vita vikali kati ya nchi hizo mbili katika siku za nyuma ambapo Argentina iliisababishia Uingereza hasara kubwa.

Ni nchi zilizonauadui uliokithiri hivyobasi kupingana vikali kutokana na uhusiano mbaya baina yao, uhusiano huo ambao ni mbaya zaidi ule wa nchi ya India na Pakistani. Wanasherehekea nchini Argentina ambapo si kitendo cha kibinadamu kusherehekea kifo cha mtu lakini wakati huo huo haifai kuhuzunika.

Kwa taifa la Pakistani hakuna uhalali wowote wa kueleza huzuni kwa sababu ukiangalia historia ya karibu na nyuma madhara na uharibifu mkubwa unaofanywa kwa Waislamu duniani kote yanatokana na Uingereza, jumuiya ya Kiingereza na familia hii ya kifalme haiwezi kulinganishwa na taifa lingine lolote. Ardhi hii imethibitika kuwa nchi ya dalili mbaya kwa Waislamu.

Kwa upande mmoja Waislamu wanadai kumiliki Uislamu kama imani na wako tayari kufa kwa ajili ya Uislamu lakini wakati huo huo wana hisia na kueleza huzuni kwa maadui wa Uislamu.

Uhalifu wa Uingereza na familia ya kifalme

Ukianza kutoka zamani sana basi uhalifu wa Uingereza na familia hii ya Kifalme unaweza kuorodheshwa kama:

  1. Salman Rushdie ambaye alimkashifu Mtukufu Mtume (s) alipewa hifadhi na Uingereza.

 

  1. Bibi mwenye kufedhehesha kutoka nchi ya Bangladesh ambaye alimtukana Mtume (s), Uislamu na mambo matakatifu ya Uislamu alipewa hifadhi na Uingereza.

 

3.Kila kitendo kinachofanywa dhidi ya dini ya Kiislamu hunafanywa chini ya hifadhi ya Uingereza.

 

  1. Ukiangalia karne moja walichofanya kwa Waislamu utagundua ya kwamba wamewadhalilisha na kuwatukana na kuwadhofisha Waislamu

 

  1. Kwa ajili ya madaraka hawakuvumilia tawala kubwa za Kiislamu za Dola ya Ottoman na kuzigawanya vipande vipande kwa msaada wa washirika wao wahaini Waarabu.
  2. Kisha wakaigawa ile dola iliyovunjika mikononi mwa hao hao Waarabu wasaliti. Na baada ya khiyana hii iliyofanywa kupitia kwa Waarabu waliwafanya watekeleze khiyana nyingine kubwa zaidi.

 

  1. Usaliti mkubwa zaidi kwa Waislamu ni kuwepo kwa Israeli. Uingereza ilifanya jambo hili lililolaaniwa katika ardhi takatifu ya Palestina.

 

  1. Waliwakusanya Wazayuni kutoka kote ulimwenguni na wakaiteka ardhi ya Palestina kwa msaada wa Waarabu hao hao wasaliti. Na leo wamewafanya Waarabu waikubali Israeli na kuwafanya kuwa watumishi wa Israeli

 

  1. Uingereza hiyo hiyo imeipora dunia nzima. Malkia huyu aliyekufa alikuwa miongoni mwa watu tajiri zaidi duniani. Utajiri wa familia ya kifalme ya malkia unaweza kuwa zaidi ya utajiri wa serikali ya Uingereza. Utajiri huu wote ulitoka wapi, walipora India, Waarabu na nchi za Kiafrika. Pamoja na utajiri huu wote uliopatikana kwa kupora na kuiba familia hii ya kifalme ilianzisha nguvu zao wenyewe.

 

  1. Ni historia ya kweli kwamba wametuma majasusi wao ndani ya nchi za Kiislamu ili kuunda makundi na madhehebu yenye itikadi kali ndani ya Waislamu. Bin Salman amekiri kwenye chaneli ya televisheni ya kwamba kwa maelekezo ya Waingereza tulifanya madhehebu yenye msimamo mkali (Uwahabi). Muundo wa madhehebu haya tulipewa na wao ambao ulizingatiwa kuwa ni hitaji la wakati. Na sasa anasema kwamba leo hakuna madhehebu au dini ya kitaifa nchini Saudi na tunatengeneza madhehebu mapya ambayo yangekubalika kwa nchi za magharibi na ulimwengu mzima wa kiliberali. Haya yote yalifanywa na Briteni kwa uwazi na ushahidi wa kihistoria upo wazi juu ya haya.

 

  1. Vile vile walipigana vita na wakajenga uadui baina ya Waislamu. Walipanga njama za vita na mabishano kati ya Shia na Sunni. Walichochea mifarakano baina ya Waislamu na hili lilifanywa kwa mbinu maalum ambayo inatumika hadi leo.

 

  1. Hivi karibuni walianzisha kikosi cha ISIS ambacho wengi wao walitoka Uingereza. Vijana wa Kiislamu nchini Uingereza na Ulaya walitayarishwa na kambi za mafunzo ziliandaliwa nchini Bosnia. Walianzisha mapango huko Uturuki. Qatar ili kuwaangamiza Mashia nchini Syria, Lebanon, Iraq na kuwakamata na kuharibu maeneo matakatifu ya Ziara. Na wakashindwa na hila ya Mwenyezi Mungu, na wakafedheheka na kufedheheshwa. Vile vile chanzo cha kila fitnah ya duniani katika nchi hii, familia yao ya kifalme ipo na ndio mtendaji wa haya yote.

 

  1. Kama alivyosema Kiongozi Mkuu Ayatullah Khamenei, wakala wa Uingereza asiyenahadhi MI6 aliunda madhehebu ndani ya Ushia ambao kazi yao ilikuwa ni kuleta mifarakano ndani ya Mashia, kueneza chuki na kufanya kufuru dhidi ya maeneno matakatifu.

 

  1. Hata hivi leo kila mhalifu wa Pakistani amesamehewa nchini Uingereza. Altaf Hussain, adui wa Pakistani ambaye uamuzi wa mahakama upo kwamba hakuna kitu chochote kutoka kwake kinaweza kutangazwa yuko chini ya kimbilio la Uingereza. Nawaz sharif ambaye ana kesi na mahakama amejihifadhi nchini Uingereza. Wazungumzaji wa kidini, wasemaji wanaozua mifarakano wako Uingereza. Vituo vya Televisheni vinavyochochea chuki vinafanya kazi kutoka Uingereza. Wale wote waliolaaniwa wanaofanya Kukufuru utakatifu kama Rushdie wako Uingereza.

Vitendo vyote hivi ni vile ambavyo Uingereza inavifanya na inavifanya na vimeufanya uadui dhidi ya Waislamu na Uislamu kufikia kilele chake.

Waliifanya Pakistani kuwa mtumwa na leo Pakistan imezingirwa chini ya madeni ya IMF kutokana na Marekani na Uingereza. Pakistan iko chini ya shinikizo la FATF ni kutokana na nchi hizi mbili.

Kwa vile Pakistan ni mwanachama wa nchi za Jumuiya ya Madola na Uingereza ndio kichwa chake basi kwa nini hawatatui tatizo hili la nchi wanachama wao badala yake kuwawekea shinikizo.

Ikiwa tutazingatia kwa pamoja tutadungundua ya kwamba nchini Pakistan uharibifu uliofanywa na Wahindu japo ni mkubwa lakini sio hata chembe ikilinganishwa na yale ambayo yamefanywa na Uingereza dhidi ya Waislamu na dhidi ya Pakistan. Wamewezaje kulifanya hili?

Nguvu laini za Uingereza

Ni istilahi zinazotumiwa na wao tu. Ni waandishi wao wenyewe walioandika kwamba Uingereza ilikuwa na nguvu zamani na hata leo. Mamlaka ambayo Uingereza ilikuwa nayo hapo awali yalikuwa na nguvu ngumu lakini leo wana nguvu laini.

Kwa nguvu ngumu waliiteka India na kuunda ubeberu kwa kuteka ulimwengu kwa nguvu zao na kampuni za biashara. Ni katika historia ambapo Uingereza haikuteka India kwa nguvu zao bali kupitia kampuni ya biashara ambayo ilikuwa kampuni ya East India.

Wahindi na Wapakistani hawawezi kamwe kujisafisha kutokana na uchafu huu kwamba jinsi walivyokuwa dhaifu na rahisi kiasi kwamba walitekwa na kampuni ya biashara na wala sio jeshi la kivita.

Waliichukua nchi hii yote kwa udanganyifu na kisha kuiteka baada ya hapo kwa muda mrefu, na kisha wakaipora nchi yako; na kuichafua elimu yako na kuangamiza kizazi chako alafu wakaondoka, lakini kwa nini Pakistani bado ni mtumwa wao na iko chini ya huzuni?

Ni nguvu gani imefanya hivi? Ni kwa nguvu laini ambapo hakuna jeshi au kampuni ya biashara ambayo inakuja na kutawala. Kwa nguvu laini udhaifu wa jumuiya huzingatiwa na kwa kuzingatia kwamba unajionyesha kuwa unavutia kiasi kwamba wanakuwa waangalifu.

Nguvu laini huwafanya wengine kuwa wapenzi wako na hii ilipatikana na Uingereza chini ya uongozi wa malkia huyu.

Mgogoro wa sasa nchini Pakistan ni kwamba uchumi unaharibiwa, ukosefu wa utulivu wa kisiasa upo na kila mtu anaonekana kuchanganyikiwa na hawezi kamwe kudhihirisha hasira zake.

Haya yote yametokea kupitia Uingereza. Huyu mtu maarufu (Imran khan) alitoka wapi? Alikuja kutoka Uingereza. Familia ya wafua dhahabu wanatoka Uingereza na walitayarisha bidhaa hii.

Wakati wowote fitna inapoanzishwa kupitia uongozi wa kidini wanaalikwa Uingereza ambako maelewano na makubaliano yote hufanywa na kisha kutumwa Pakistani.

Tamaa ya Pakistani kwa Uingereza

Nchi ya watumwa ya Uingereza kama Pakistan inapaswa kuwa na chuki dhidi yao lakini wamefanya mamlaka yao laini ya kuvutia kiasi kwamba Wapakistani wamerogwa. Leo hii kila Mpakistani ana tamaa na mapenzi kwa Uingereza.

Wanajivunia kuwatuma watoto wao na kuishi Uingereza. Tulipaswa kuwa na aibu, kuhisi hatia na kwa hakika Mpakistani hakupaswa hata kusafiri na shirika la ndege linalopaa juu ya Uingereza.

Ni kwa sababu wametukana dini yetu, elimu, manabii na kuwadhalilisha Waislamu. Wametunyang’anya Palestina, wamewagawanya Waislamu na kila balaa limetoka kwao tu.

Mbweha wa kale amekufa

Jina ambalo Imam Khomeini (r.a) alilitumia kwa Uingereza ndilo lililofaa zaidi ambalo lilikuwa ni “Mbweha Mkongwe”. Angeiita Amerika kwa jina la Mbwa mwitu ambaye alitumia nguvu na Uingereza ni mbweha wa zamani ambaye anafanya udanganyifu. Ikiwa leo hii mbweha amekufa basi msitu unapaswa kuhuzunishwa na kifo chake.

Mataifa ya Jumuiya ya Madola ni msitu ule ambao chifu wake hakuwa simba bali ni mbweha mkongwe na sehemu moja ya msitu huu ni Pakistan. Ni aibu kwa Pakistan kubaki kama mwanachama wa nchi za jumuiya ya watumwa na kujifakharisha juu ya hilo.

Hatupaswi kusherehekea kama vile Argentina ambayo si kitendo cha kibinadamu kwa kifo cha mtu yeyote lakini tunapaswa hata kuwa na huzuni kuhusu ardhi hiyo na familia ya kifalme ambayo ni familia iliyolaaniwa zaidi.

Kwa nini Uingereza imeifanya familia ya kifalme kuwa yenye heshima?

Sasa nitataja mwelekeo mmoja zaidi kuhusu familia hii ya Kifalme kwa nini familia hii ina hadhi ambapo Uingereza ni taifa la kidemokrasia na lililoendelea. Kwa hiyo, kwa nini wamehifadhi magofu ya familia hii ya kifalme hadi sasa? Hili ni muhimu sana kwa Waislamu na Wapakistani kuelewa jambo hili.

Nchini Uingereza mamlaka iko kwa serikali ya kidemokrasia na ufalme huu wa familia ya kifalme uko chini ya sheria na sio juu ya sheria kama familia ya kifalme ya Saudi Arabia iko juu ya sheria na wanadhibiti sheria lakini sio Uingereza.

Ufalme umehifadhiwa nchini Uingereza ingawa hii imeisha ulimwenguni kote na kuna utajiri mkubwa unaotumiwa kwa familia hii. Utajiri huu hautokani na kodi za watu wa Uingereza bali ni utajiri ulioporwa kutoka nchi nyingine kama vile Waarabu na mataifa mengine. Kashfa moja ni kuhusu Prince Charles, ambaye ni mtoto wa miaka 73 wa Malkia huyu.

Amechukua mamilioni ya dola kutoka kwa kaka yake Bin Laden magaidi kwa jina la ustawi. Familia hii ya kifalme inafanya kazi kupitia mapato haramu ambayo mengine ni moja kwa moja chini ya ustawi wa Kifalme na mengine hufanywa kupitia serikali ya Uingereza. Namkumbuka kijana mmoja ambaye kwa njia fulani alifika Australia kwa taabu nyingi na hatimaye akapata makazi kwenda Australia na kisha akarudi Pakistani kupitia Qom kukutana nami.

Nilimwambia ni nini kilichokuwa hitaji kubwa kwako kuja hapa tukutane. Alisema nimekuja hapa kukuambia kwamba ulichokuwa ukiniambia hapo awali sitakisikiliza kwa sababu nililogwa na mapenzi ya Australia.

Alisema siku moja tulikuwa tunakula chakula kwenye kambi ya wakimbizi huko Australia na wakaniambia kuwa unajua chakula hiki kinatolewa kwa bajeti gani na gharama zote za watu hawa hutunzwa katika kambi hizi. Alisema niliwaambia itakuwa kutoka kwa ushuru wa watu.

Waliniambia hapana sio hivyo lakini badala yake huko Australia kuna ushuru maalum kwa makahaba ambao wamewawekea wahamiaji wanaokimbilia.

Huyu kijana alisema nilianza kutapika eti nakula pesa gani? Kuanzia siku hiyo nilianza kupiga kelele za kurudi lakini walikuwa hawanirudishi, kisha baada ya mabishano kadhaa wakanirudisha.

Bajeti inayotolewa kwa familia ya kifalme ni uporaji wa pesa zisizo halali. Kwa nini nchi iliyoendelea, ya kisasa kama Uingereza imehifadhi magofu haya ya familia ya kifalme.

Hii ni kwa sababu familia hii ni ishara ya ufalme wa Uingereza na utawala wa ulimwengu. Uwepo wa familia hii unaonyesha kwamba jina la Uingereza lilitokana na familia hii na nchi walizoziteka, waliharibu mataifa mangapi. Wamehifadhi magofu haya kama heshima kwa familia ya kifalme na ni kwa kiasi gani wamepora ulimwengu na kuzipeleka mali hizo Uingereza. Sasa wana mila zisizo na msingi, zisizo na maana ambazo utaona wakati wa mazishi yake ni jinsi gani watafanya mambo yasio na msingi. Hii ni familia kubwa na takriban theluthi moja ya Uingereza ni mali za familia hii na mbali na kwamba mapato haya yanafikia familia hii kutoka Australia, Pakistan na mataifa mengine, Wameiweka familia hii kama picha ya nguvu ya kibeberu ya Uingereza. Waingereza wamevumilia mambo yote yasiyo na maana, yasiyo na maana ya familia hii. Kizazi kipya cha Uingereza hakijali jinsi Uingereza ilivyokuwa huko nyuma lakini wanajali zaidi hali ya sasa ya Uingereza na kwa hili wameanzisha harakati nchini Uingereza ya kutaka kumaliza familia ya Kifalme. Wanataka kusitisha gharama zote za familia hii na inakadiriwa kuwa baada ya kifo cha Malkia harakati hii itazidisha kasi yake ili kuimaliza familia hii milele. Wanataka kuondoa mzigo na matumizi ya ziada kutoka Uingereza.

Minyororo na Pingu laini za vyombo vya habari vya Pakistan za utumwa wa Uingereza

Vyombo vya habari vya kufedhehesha vya Pakistani kwa mwaka mzima vinazungumza kuhusu wana wa Diana. Prince amefanya kitu flani au amebaka mtu au ametembelea sehemu fulani. Je, kuna haja gani ya kutoa habari kuhusu familia hii chafu kwa Wapakistani? Hii ni ishara ya utumwa na vyombo vyetu vya habari vinapaswa kukuza kujistahi na kufikiria wamefanya nini na sisi. Wametudhalilisha na maswala yote ya sasa mnayovuna yalipandwa na wao. Madhehebu, mifarakano, udhalilishaji yote yanatokana na wao na lugha hii ya kiingereza mliyoikumbatia ni pingu laini za huyu jamaa shingoni mwenu na mnavifanya vizazi vyenu viwe vipenzi vyao. Mwenyezi Mungu atujaalie utu na atutoe katika utumwa huu.

 

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *