Vifo na uharibifu, matokeo ya utawala wa Kizayuni wa kuivamia kambi ya Balata

Maelfu ya Wapalestina walizika miili ya mashahidi Fathi Jihad Abd Salam Rizk, umri wa miaka 30, Abdullah Yusuf Muhammad Abu Hamdan, umri wa miaka 24 na Muhammad Bilal Muhammad Zeitoun, waliouawa shahidi katika shambulio la utawala wa Kizayuni kwenye kambi ya Balata huko. mashariki mwa Nablus.

Idadi ya Wapalestina wengine pia walijeruhiwa katika mapigano makali katika kambi ya Balata. Wazayuni pia waliharibu baadhi ya nyumba kwa kisingizio kwamba vilipuzi vilifichwa ndani yake.

Mashuhuda wa tukio hilo walisema kuwa wanajeshi hao wa Kizayuni walizuia gari la wagonjwa kuingia mahala hapo kuwasafirisha majeruhi hao. Wakati huo huo, idadi nyingine ya vikosi vyao ilianza kuharibu nyumba za watu kwa kisingizio cha kugundua ghala la vilipuzi.

Waombolezaji hao wameuomba muqawama wa Palestina uendelee kusimama dhidi ya uvamizi wa utawala huo ghasibu wa Kizayuni ambao umekuwa ukiimarishwa ili kuwaridhisha wakufurishaji wa utawala huo ghasibu. Pia walitangaza mgomo mkuu huko Nablus jana.

Wakati huo huo, Chama cha Wananchi kwa ajili ya Ukombozi wa Palestina kimesisitiza kuwa, ” jinai za utawala huo ghasibu dhidi ya taifa letu na maeneo yetu matakatifu hazikosi bila jibu, na wananchi na muqawama wa Palestina daima wamethibitisha ukweli huo.” “Jinai za utawala wa Kizayuni katika miji, vijiji na kambi Zetu ni thibitisho la kushindwa kwa utawala huu kupinga muqawama wa wananchi wetu.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *