Raia huyo wa Palestina aliuawa shahidi kutokana na kukithiri kwa majeraha aliyoyapata katika mashambulizi ya wanajeshi wa Kizayuni katika kambi ya Jenin.
Wizara ya Afya ya Palestina katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan ilitangaza kuwa, raia mmoja wa Palestina aliuawa shahidi wakati wa mashambulizi ya wanajeshi wa Kizayuni katika kambi ya Jenin iliyoko kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
Wakati huo huo duru za ndani za Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan zimeripoti kuuawa shahidi kijana wa Kipalestina huko Salafit, kwa kupigwa risasi na walowezi wa Kizayuni.
Kufuatia shambulio la Wazayuni dhidi ya Jenin, kumetokea mzozo mkali wa silaha kati yao na wapiganaji wa muqawama. Vyanzo vya Palestina vimeripoti kwamba Wazayuni waliizingira nyumba ya Zakaria al-Zubaidi, na hatimaye wakamkamata kaka yake Jabreel al-Zubaidi.
Wizara ya Afya ya Palestina imetangaza kuwa, Wapalestina 3 wamejeruhiwa katika shambulio la Wazayuni katika kambi ya Jenin.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Palestina, vikosi vya muqawama katika kambi hiyo viliwalenga wanajeshi wa Kizayuni kwa kuwafyatulia risasi na kutumia vifurushi vya milipuko, na matokeo yake Wazayuni kadhaa walijeruhiwa.