Kiongozi wa HAMAS: Mazingira ya Ukingo wa Magharibi ni utangulizi wa kuutokomeza utawala wa Kizayuni

Mjumbe wa ofisi ya kisiasa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema mazingira ya hivi sasa katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan ni utangulizi wa kutokomezwa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel.

Mahmoud Az-Zahar ameongeza kuwa, nchi kama Syria, Lebanon na Palestina ambazo zimedhuriwa na utawala wa Kizayuni, inapasa zisimame pamoja kwa msaada na uungaji mkono wa nchi kama Iran, Iraq na Yemen ili kuutokomeza utawala huo haramu.

Kiongozi huyo mwandamizi wa Hamas amesisitiza kuwa Muqawama ulichukua hatua kwa msingi wa kujihami na kwa kutumia nyenzo zote sambamba na kuziimarisha na kuzistawisha nyenzo hizo hususan katika Ukanda wa Gaza na kwamba hatua hizo zilipelekea kutimuliwa utawala huo ghasibu huko Gaza.

Az-Zahar amebainisha kuwa, Wapalestina, hususan wale wanaoamini kuwa ukombozi wa ardhi yote ya Palestina utapatikana kupitia Muqawama wamesimama kwa mapambano na akaongeza kuwa, kujitoa mhanga na kufa shahidi kunafanyika kwa ajili ya kufikia lengo lililokusudiwa ambalo ni kuutimua utawala ghasibu wa Kizayuni katika ardhi ya Palestina.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *