Katika Hotuba yake ya Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, Ayatullah Ali Khamenei alizungumza katika siku hii inayosadifiana na Siku ya Kimataifa ya Quds iliyorushwa moja kwa moja na kupitia televisheni akisema;
‘Salamu kwa taifa lao kuu la Iran, ambalo limeunda historia siku hii ya leo na kubainisha maana ya kweli ya neno hamasa, Salamu na amani ziwe juu ya Imamu Mwendazake Aliyeadhimu ambaye ni mwanzilishi wa msingi huu wenye baraka leo hii na katika siku zijazo.
Kuwepo kwa watu katika Siku hii ya Al-Quds kwa hakika limekua jambo lenyekuleta hamasa na mwamko, na harakati hii maarufu ni kazi kubwa na yenye baraka, na uwepo wa watu ni moja kati ya harakati muhimu za kisiasa na zenye kuihami Al-Quds.
Wanaopapambana kuitetea Al-Quds ilioko Palestina hii leo watapata nguvu zaidi kwa kuungwa mkono na mataifa, na hatimaye kufikia natija iliyobora.
Wale wanaotetea Al-Quds na Msikiti wa Al-Aqsa, kibla cha kwanza cha Waislamu, kwa miili na roho zao leo, watatiwa moyo na harakati hii ya taifa la Iran, na watapata nguvu na uvumilivu.Matokeo yake ya mwisho, ambayo yalikuwa matokeo yenye baraka, yatakuwa karibu na mafanikio ya kimungu.