Kizazi cha Waingereza weusi chapoteza imani kwa polisi wa nchi hiyo

Matokeo ya utafiti uliofanywa nchini Uingereza yanaonyesha kiwango kikubwa cha kutokuwa na imani kizazi cha vijana weusi wa nchi hiyo kwa polisi; Kwa kadiri kwamba hawataki hata kupiga simu polisi wakatii wa hatari.

Kulingana na matokeo ya utafiti wa shirika la ushauri la Uingereza, Crest, asilimia 36 tu ya vijana weusi ndio waliosema kuwa wanawaamini polisi wa nchi hiyo.

Hii ni wakati ushahidi umethibitisha kuwepo mienendo ya kibaguzi ya polisi wa Uingereza dhidi ya watu waliowachache kirangi, kikaumu na kidini.

Utafiti uliofanywa na gazeti la Guardian nchini Uingereza mnamo Agosti 2022 unaonyesha kuwa  uwezekano wa kutozwa faini kaumu za waliowachache nchini humo ni mara mbili zaidi ya wazungu.

Utafiti huo umebaini kuwa, katika suala la matumizi ya nguvu na ukatili, polisi wa Uingereza hufanya ubaguzi na kutofautisha baina ya wazungu na watu wa rangi na mbari nyingine.

Takwimu za 2020 zinaonyesha kuwa nchini Uingereza, utumiaji wa bunduki dhidi ya raia weusi ulikuwa mara nane zaidi kuliko watu weupe mnamo 2018-2019.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *