Moja ya matukio ya kuvutia katika michuano ya Kombe la Dunia nchini Qatar ni kukataa wananchi wa mataifa mbalimbali ya Kiarabu kuhojiwa na vyombo vya habari vya Israel na vilevile kuiunga mkono Palestina dhidi ya utawala huo wa Kizayuni.
Kanali ya 12 ya utawala wa Kizayuni imeweka wazi katika ripoti yake kwamba, kwa Watunisia, Palestina ni muhimu zaidi kuliko kitu chochote katika Kombe la Dunia. Mashabiki wengi wa timu ya Tunisia hushiriki katika maandamano ya kuunga mkono taifa la Palestina na wakati wa michezo hiyo, wanafikisha ujumbe wa kuliunga mkono taifa la Palestina na kubeba mabango kwenye viwanja vya soka yenye kaulimbiu ya ukombozi wa Palestina, mpaka baadhi yao wanayachukulia mashindano ya Kombe la Dunia kuwa ni fursa mwafaka ya kuwatangazia na kuwabainishia walimwengu habari na matukio ya Palestina.