Kremlin: Russia itatumia silaha za nyuklia uwepo wake ukitishiwa

Ikulu ya Russia ya Kremlin imesema nchi hiyo haitakuwa na chaguo jingine isipokuwa kutumia silaha za nyuklia iwapo uwepo wa taifa hilo utakabiliwa na vitisho.

Msemaji wa Kremlin, Dmitry Peskov alisema hayo jana Jumanne katika mahojiano na kanali ya televisheni ya CNN na kueleza kuwa, nchi hiyo haina azma ya kutumia silaha za nyuklia, lakini kanuni za nchi hiyo kuhusu matumizi ya silaha hizo zipo wazi.

Amebainisha kuwa: Iwapo usalama wa ndani utakuwa hatarini, basi tunaweza kutumia silaha hizo (za nyuklia) kwa mujibu wa sheria na kanuni zilizopo.

Peskov amesisitiza kuwa, Russia haina sababu ya kutumia silaha hatari za nyuklia iwapo usalama wa taifa hilo hautakuwa katika hatari.

Siku chache zilizopita, Russia ilitumia kwa mara ya kwanza kombora la kistratijia la Hypersonic la Kinzhal katika vita vyake na Ukraine.

Makombora ya Kinzhal ni miongoni mwa silaha za kimkakati za hali ya juu zaidi za Russia na yalizunduliwa rasmi Rais Vladimir Putin mwaka 2018.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *