Wajumbe wa Israel waliokuwa wameingia kisiri katika ukumbi wa mikutano wa viongozi wa Umoja wa Afrika walifukuzwa kutoka katika mkutano huo.
Shirika la habari la Palestina “Shahab” lilichapisha video ya kufukuzwa kwa ujumbe wa Israel katika ukumbi wa mkutano wa Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, ujumbe wa utawala wa Kizayuni uliingia kwa siri katika ukumbi wa mikutano wa viongozi wa Umoja wa Afrika na kuongozwa nje ya ukumbi huo na vikosi vya usalama.
Mkutano wa 36 wa wakuu wa Umoja wa Afrika ulianza Jumamosi ukiwa na kauli mbiu “Harakisha uundaji wa Eneo Huria la Biashara la Afrika”.