Utafiti mpya uliofanywa unaonyesha kuwa, vitendo vya kubakwa wanawake na kunyanyaswa kingono vimekithiri katika jeshi la Uingereza.
Utafiti huo unaonyesha kuwa, ni kwa miaka 20 sasa ambapo wanawake wamekuwa wakibakwa na kunyanyaswa kingono katika Chuo cha Mafunzo ya Jeshi la Sandhurst nchini Uingereza na matukio ya karibuni kabisa ni ya mwezi uliopita wa Novemba.
Gazetii la Daily Mail linaripoti kuwa, matukio ya kubakwa na kunyanyaswa kingono wanafunzi wa kike wanaokwenda kupata mafunzo ya kijeshi katika Chuo cha Jeshi cha Sandhurst yamekuwa yakitokea mara kwa mara na kufikia hatua ya kuwa jambo la kawaida.
Daily Mail linanukuu simulizi za msichana mmoja ambaye amepitia mafunzo ya kijeshi katika chuo hicho akieleza kwamba, maafisa wa jeshi ambao ni wasimamizi wa mafunzo katika chuo hicho walikuwa wakiwabaka na kuwanyanyasa kingono.
Ripoti mbalimbalii zinaonyesha pia kuwa, uraiani nako hali si shwari kwani vitendo vya ubakaji vimeongezeka katika jamii ya Uingereza na kuonyesha ni kwa kaisi gani nchi hiyo ya bara Ulaya inakabiliwa na mmomonyoko wa kimaadili.
Kituo cha taifa cha takwimu nchini Uingereza kimetangaza kuwa, vitendo vya ubakaji na unyanyasaji wa kingono vimeongezeka nchini humo kwa kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa.
Kwa mujibu wa kituo hicho cha taifa cha takwimu cha Uingereza, matukio ya ubakaji yanachangia asilimia 37 ya kesi zote za uhalifu wa unyanyasaji wa kingono zilizoripotiwa katika idara ya polisi.