Kundi la Saba: Tunaunga mkono kurefushwa kwa mda wa usitishaji vita mjini Gaza

Katika taarifa ya pamoja, mawaziri wa mambo ya nje wa nchi zenye uwanachama wa G7 waliunga mkono kurefushwa kwa usitishaji vita katika Ukanda wa Gaza na kuendelea kwa usitishaji huo wa kibinadamu.

Kwa mujibu wa ripoti ya kundi la kimataifa la shirika la habari la Fars, katika muendelezo wa uungaji mkono wa nchi za Magharibi na mashirika ya kimataifa kwa ajili ya kurefusha usitishaji vita wa muda katika Ukanda wa Gaza, Kundi la 7 pia lilitaka kuendelezwa kwa usitishaji huo wa kibinadamu.

Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi wanachama wa G7 walisema katika taarifa yao Jumatano asubuhi: “Tunaunga mkono kurefushwa kwa usitishaji vita kati ya Hamas na Israel na makubaliano ya mapumziko ya siku za usoni ikiwa ni lazima, kuongeza msaada unaotumwa katika Ukanda wa Gaza na kuachiliwa kwa mateka wote.”

“Tunatoa wito kwa Houthis kuacha mara moja mashambulizi dhidi ya [Israeli] na vitisho kwa meli za kimataifa na kuachilia meli ya Galaxy Leader na wafanyakazi wake,” ilisema taarifa hiyo.

Mawaziri wa mambo ya nje wa Kundi la 7 pia wameongeza: “Tunashukuru juhudi za Marekani, Qatar na Misri za kukomesha uhasama na kuunga mkono juhudi za Umoja wa Mataifa za kutoa msaada.”

Hapo awali, Rais wa Kamisheni ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen Jumanne asubuhi alikaribisha makubaliano ya kurefusha usitishaji vita wa muda katika Ukanda wa Gaza kwa siku mbili.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *