Kupungua idadi ya Wakristo Magharibi kwaibua changamoto kwa viongozi wa kidini

Kumeibuka mjadala mpya katika nchi za Magharibi kuhusu kuporomoka kwa dini ya Kikristo baada ya sensa ya Waingereza kufichua kwa mara ya kwanza kwamba idadi ya wafuasi wa dini hiyo huko Uingereza na Wales imepungua na kufikia chini ya nusu ya idadi ya watu. Suuala hili pia imeshuhudiwa hivi karibuni huko Marekani, ambayo ni mojawapo ya nchi za Magharibi za kihafidhina.

Jambo hili limetajwa na wachambuzi wa mambo kuwa ni kiashiria cha mabadiliko makubwa katika utamaduni wa Magharibi, na kielelezo cha kutoweka “ustaarabu wa Kikristo”.

Mwishoni mwa mwezi Novemba, Ofisi ya Taifa ya Takwimu ya Uingereza ilichapisha matokeo ya sensa inayofanyika kila baada ya miaka 10, ambayo yanaonyesha kuwa asilimia ya wale wanaojieleza kuwa Wakristo nchini Uingereza na Wales haizidi 46.2 ikilinganishwa na 59.3% iliyorekodiwa katika sensa ya awali ya 2011. Takwimi hizi zinaonyesha kushuka kwa kiasi kikubwa kwa idadi ya Wakristo katika kipindi cha muongo mmoja tu.

Kwa upande mwingine asilimia ya watu wasioamini dini katika sensa hiyo – iliyofanyika mwaka jana na kutangazwa hivi karibuni – ilipanda hadi 37.2 ikilinganishwa na 25% miaka 10 iliyopita. Matokeo ya sense hiyo yanaonyesha kuwa idadi ya Waislamu imeongezeka kutoka asilimia 4.9 mwaka 2011 hadi asilimia 6.5.

Mwezi Septemba mwaka huu pia, uchunguzi mkubwa uliofanywa na Kituo cha Utafiti cha Pew ulifichua kwamba idadi kubwa ya kizazi kipya na cha vijana wa Marekani wanaacha Ukristo.

Ripoti ya awali ya uchunguzi uliofanywa na kituo cha utafiti cha Pew Research Center cha Marekani ulionyesha kuwa, Uislamu ndiyo dini kubwa inayokuwa na kuongezeka kwa kasi duniani ikilinganishwa na dini nyingine.

Kituo hicho cha utafiti cha Marekani kimesema katika ripoti hiyo kwamba, hadi kufikia mwaka 2070, Uislamu utakuwa dini kubwa zaidi ulimwenguni.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *