Kutoa sadaka kila kitu ulicho nacho kwa ajili ya kumpenda Mwenyezi Mungu ni dhabihu:Allama Syed Jawad Naqvi

Eid Al Adha – 10th July 2022

 Hujjatul Islam Ustad Syed Jawad Naqvi

 (Mkuu wa shule Jamia Orwatul Wuthqa – Lahore)

 Imetolewa: Msikiti wa Baitul Ateeq

 Lahore – Pakistan

 

Hotuba ya 1: Kutoa sadaka kila kitu ulicho nacho kwa ajili ya kumpenda Mwenyezi Mungu ni dhabihu

Taqwa ni kinga kutoka kwa Mwenyezi Mungu ambayo imewasilishwa katika Quran na kuhubiriwa kupitia Mtume na kukabidhiwa kwa Maimamu na kisha wanachuoni kwa ajili ya kuimarisha Msingi huu (Taqwa) na kusimamisha mfumo wa Taqwa.

Matukio mahsusi ambayo Taqwa inahitaji kukuzwa na kufundishwa kwa waumini ni swala ya Ijumaa ambayo ndio ya kwanza kabisa na kisha Siku ya Eid. Natoa pongezi na salamu zangu kwa Ummah mzima kwa kumuomba Mwenyezi Mungu atujaalie kuielewa njia iliyoyasawa na kwamba atujaalie sote fursa ya kusimamisha umoja na kutekeleza mafundisho ya dini.

Ni wazi kwamba swala ya Idi ni wajibu kwa wasiokua mashia japo kwa mashia kumekuwa na shaka ambayo imethibitisha kwamba katika kipindi cha ughaibu wa Imamu wa zama (a.j) Idi sio wajibu kamwe. Nimelifafanua hili katika hotuba za swala ya Ijumaa na ndivyo hali ilivyo katika siku ya Idi. Mafaqihi wote wanakubaliana ya kwamba anapohudhuria Imamu maasumu (asiyekosea) swala ya Idi ni wajibu na kama hatokuwepo basi ni hiari kuswaliwa au itatekelezwa kama amali iliyopendekezwa.

Tumekanusha hili hapo mwanzoni kwa maelezo na kwa ufafanuzi zaidi na kama Sira ya Maimamu pia ilitakiwa kusomwa kama faradhi, basi waumini watafanya matendo yao kwa mujibu wa hukumu za Mujtahid wao.

Kuna Idi mbili muhimu, ya kwanza ni Fitr na ya pili ni Eid-al-Adha. Ibada muhimu inayohusiana na Eid al Adha ni dhabihu (qurbani) ambayo inatokana na neno ‘qurb’ ambalo linamaanisha ukaribu. Ni njia ambayo kwayo tunajikurubisha kwa Mwenyezi Mungu kama kitendo cha Muumini. Na katika hadithi imebainishwa kwamba swala kwa kila Muumini ni ‘qurbani’ kwa sababu tunamkaribia Mwenyezi Mungu.

Kutoa sadaka na kafara ya wanyama iko katika kundi moja. Ikiwa unafanya Hija ukiwa Makka basi kutoa kafara ya mnyama kama ‘qurbani’ (dhabihu) ni wajibu lakini kwa asyekuwa Makka basi si wajibu japo imesisitizwa kwa waumini na Maimamu kufanya kitendo hiki na kujikurubisha kwa Allah (s.w.t.).

Kwetu sisi faida zinajulikana, ambapo dhabihu hizi zote zinapaswa kuwa ni faida kwa jamaa, jirani na watu masikini.Ijapokuwa Mwenyezi Mungu ameelezea kila kitu kwa uwazi, lakini wanazuoni hutaka kuficha mambo, baadhi yao hawapendi kuona watu wanaelezewa kila jambo katika dini.

Kila kilichomo ndani ya Quran ni haki kwa watu kukijua. Ibada zilizoashiriwa na Qur’an au Mtume (s.a.w.w.) zina taswira ya hali, mazingira ya zama hizo. Vilevile ahkam (sheria) hizi zilibainishwa kwa kuzingatia hali ya zama hizo. Wakati huo nyama haikuwa sehemu ya chakula cha kila siku kutokana na hali ya kiuchumi. Matajiri walikuwa na matumizi ya nyama nyingi kwenye menyu yao lakini kwa watu wa kawaida tende ndio ilikua chakula cha kawaida. Ilikuwa ni vigumu kwao nyama kuwafikia. Leo hii nyama imekuwa chakula halisi kwa watu. Wakati huo nyama zingepatikana katika matukio maalum kama vile ndoa za matajiri. 

Mojawapo ya sababu zinazofanya qurbani (dhabihu) kutiliwa mkazo ilikuwa ni kutoa nyama pia kwa watu maskini. Kwa sasa ulaji wa nyama umekuwa chanzo cha matatizo ya kiafya. Hivyobasi leo hii kutoa kafara ya mnyama katika siku ya Idi haina faida sawia na ilivyokua enzi zile. Tunapaswa kuzingatia kile ambacho ni chenye manufaa kwa watu. Ingawa zipo nchi nyingi hii leo kama vile Afrika, Pakistani n.k. hazipati nyama ya kula kwa kipindi cha mwaka mzima. Wale wanaokula nyama mwaka mzima basi wasile nyama yote pekeyao na hata ikiwa nyama nzima itawafikia watu masikini basi ndivyo inavyopaswa. Kuna sehemu tatu; ya kwanza ni kwa ajili yenu, nyingine kwa ajili ya jamaa (familia) zenu na ya tatu ni kwa ajili ya masikini.

Chakula kisichowahusu watu maskini ni chakula cha hali ya chini sana. Imam Ali (a) alimkemea gavana wake wa Basra kwa kuhudhuria chakula cha jioni ambapo hapakuwa na masikini. Mfumo wa maisha ambao Ahlulbayt wametuonyesha ndio mfumo tunaopaswa kuutumia katika maisha yetu.

Kuna hekima na falsafa kwenye kafara tunayoitoa ndani ya siku hii ya Idi. Tunapata mwongozo na desturi maalum kutokana na aliyoyafanya Nabii Ibrahim katika siku hii na Mwenyezi Mungu anawaamuru waumini wote walioongoka kurudia matendo hayo (ya Nabii Ibrahim) ili waweze kudhihirisha sifa, tabia na utu wa Ibrahim. Sadaka ni sehemu ya Hija ambayo ni desturi ya Nabii Ibrahim. Qur’an imetueleza kua Nabii Ibrahim ni mfano wa kuigwa kwetu sisi na tunapaswa kumfuata kama vile wanafunzi wanavyomfuata mwalimu anayeandika ubaoni nao wanaandika hivyo hivyo kwenye vitabu vyao kwa mara kadhaa wakifanya mazoezi.

Ibrahim aliamrishwa kuondoka katika eneo lake la asili lililokua na mandhari mazuri na kuhamia kwenye nchi yenye ukame. Alikuwa mzaliwa wa mji wa Babeli na hadi kufikia sasa sehemu hiyo ingali inapatikana . Hii ni ardhi yenye rutuba yenye mito lakini hii leo watu wameifanya kuwa sehemu yenye viwanda. Natamani Lau mji wa Karbala ungebaki kama ulivyokuwa hapo awali lakini mabepari wamebadilisha kila kitu.

Nabii Ibrahim (a) aliamrishwa ahamie Makka ambayo ilikuwa sehemu isiyo na utulivu iliyopo kwenye bonde. Alimwacha mkewe na mwanawe aliyezaliwa huko miaka themanini na miwili baadae . Kisha Ismael akawa na kiu na mama yake Hajar akawa anakimbia kati ya vilima viwili huku akipiga kelele za kuomba msaada kwa sababu mtoto alikuwa karibu kufa kwa kiu. Kisha Mwenyezi Mungu akafanya muujiza wa chemichemi kutiririka chini ya miguu ya Ismael. Naye Hajar akamzoesha Ismael na kumfanya kuwa kijana, kisha Mwenyezi Mungu akamwamuru Ibrahim kutoa sadaka kutokana na kitu anachokipenda.

Ibrahim (a) alitafakari na kugundua kuwa baada ya Mwenyezi Mungu ninayempenda ni mwanangu kama ambavyo alimpata kwa dhiki baada ya shauku ya muda mrefu.

Aliwasilisha amri ya Mwenyezi Mungu kwa mkewe Hajar na yeye pia akakubali kwakua ilikuwa ni amri ya Mwenyezi Mungu. Alimwambia mwanawe Ismael naye vilevile akakubali kwa kujibu; ewe baba yangu! Tenda unavyo amrishwa, utanikuta mimi, Inshallah, katika wanao subiri. Kisha Ibrahim akaondoka kuelekea Arafa ambako aliamrishwa kumchinja mwanawe. Kisha akaja Mina na amri ilikuwa pale mahali ambapo sadaka hutolewa. Wakati wa safari Shetani alikuwa akijaribu kumzuia Ibrahim kufanya kitendo kile. Ibrahim alimpiga kwa mawe Iblis mara tatu.

Ibrahim (a) akamchukua na kumpeleka sehemu ya kuchinjia na alipokiweka kisu shingoni Mwenyezi Mungu akasema umetimiza ahadi uliyoiahidi. Kisha baada yake kondoo akaja kama mbadala na hii ikawa ndio desturi. Kila hatua na kila tendo la Ibrahim likawa ni desturi ya Hija yenye kumuimarisha Ibrahim. Sira ya Ibrahim, Hajar, Ismael (a) ikawa Hija kwetu na miongoni mwa ibada hizo ni kafara.

Katika Surah Mumtahana Mwenyezi Mungu ametuainishia yule ambaye tunapaswa kumfanya ‘Uswa’ (mfano wa kuigwa)

 

قَدْ كَانَتْ لَكُمْ أُسْوَةٌ حَسَنَةٌ فِي إِبْرَاهِيمَ وَالَّذِينَ مَعَهُ إِذْ قَالُوا لِقَوْمِهِمْ إِنَّا بُرَآءُ مِنْكُمْ وَمِمَّا تَعْبُدُونَ مِنْ دُونِ اللَّهِ كَفَرْنَا بِكُمْ وَبَدَا بَيْنَنَا وَبَيْنَكُمُ الْعَدَاوَةُ وَالْبَغْضَاءُ أَبَدًا حَتَّىٰ تُؤْمِنُوا بِاللَّهِ وَحْدَهُ إِلَّا قَوْلَ إِبْرَاهِيمَ لِأَبِيهِ لَأَسْتَغْفِرَنَّ لَكَ وَمَا أَمْلِكُ لَكَ مِنَ اللَّهِ مِنْ شَيْءٍ ۖ رَبَّنَا عَلَيْكَ تَوَكَّلْنَا وَإِلَيْكَ أَنَبْنَا وَإِلَيْكَ الْمَصِيرُ

Hakika nyinyi mna mfano mzuri kwenu kwa Ibrahim na wale walio kuwa pamoja naye, walipo waambia watu wao: Hakika sisi tumejitenga nanyi na hayo mnayo yaabudu badala ya Mwenyezi Mungu. Tunakukataeni; na umekwisha dhihiri uadui na chuki baina yetu na nyinyi mpaka mtakapo muamini Mwenyezi Mungu peke yake. Isipo kuwa kauli ya Ibrahim kumwambia baba yake: Hakika nitakuombea msamaha, wala similiki chochote kwa ajili yako mbele ya Mwenyezi Mungu. Mola wetu Mlezi! Juu yako tumetegemea, na kwako tumeelekea, na kwako ndio marejeo.

Maisha ya Ibrahim (a) na maswahaba zake ni kigezo kwanu. Ibrahim alipotangaza waziwazi kwa jamaa yake na watu wa kabila lake kwamba mimi ninajitenga na ushirikina. Sio tu kujiweka mbali na makafiri bali inapaswa kuwa na chuki dhidi ya maadui pia.

Wakati wa Hija tunahitaji kujitenga kwa kutangaza waziwazi. Saudia imekataza hili kwa kuwa na urafiki na maadui lakini Mashia wamefanya hivi kwa hiari yao ili wasijitenge na Shirki. Shirki iliyomo katika umma na nyumba zenu. Na sio kujitenga tu, bali kukataa, chuki na kupigana na maadui. wasipoiacha Shirki na kukubali tauhidi hali hii itaendelea. Jambo moja hasa kwa Ibrahim (a) lililotajwa hapa ni kama Quran inavyosema Ibrahim asiwe kigezo kwako katika jambo moja ambapo imetajwa kuhusu baba yake Ibrahim.

Neno “Ab” ni neno la jumla na halina maana sawa na  baba. Baba kwa Kiarabu ni yule ambaye  mtu amezaliwa kutoka kwenye kiuno chake. Alikuwa mlinzi wa ndani wa Ibrahim na alikuwa akimruzuku Ibrahim. Alikuwa mtu wa jamii ya wazee na alikuwa waziri mkuu wa Nimrud. Ibrahim (a) akamwambia yeye na maswahaba zake kwamba sisi tunajitenga nawe, tunakukanusha na tuna uadui nawe.

Pamoja na hayo kwa vile alikuwa mlezi, Ibrahim alisema nitakuombea msamaha. Mwenyezi Mungu alisema haya ni kwa ajili ya Ibrahim tu, lakini kwetu sisi hatuwezi kumuombea Mushrik hata awe ni baba mzazi au yeyote miongoni mwa jamaa wa karibu. yeyote atakayefanya Shirki basi hufai kuwaombea msamaha.

Katika Aya ya 6 vilevile Ibrahim ametajwa kama mfano wa kuigwa kwa Ummah. Mfano wa kuigwa wa Ibrahimu umepewa umbo la kiwiliwili. Kama ambavyo  leo hii kuna filamu zilizotengenezwa za Manabii, Mwenyezi Mungu pia ameirekodi misingi ya dini na Akachagua herufi tatu, akawachagulia mahali na kuwataka wafanye mambo fulani. Walipofanikiwa kutekeleza majukumu yao, walifanywa kuwa Maimamu na tumeamrishwa tuwafuate na kurudia kitendo kile kile cha ishara kwenye eneo lile lile na kisha mrudi na mfanye hivyo katika sehemu zenu.

Zamani palikuwa na nguzo ndogo ambayo ilitakiwa kupigwa mawe. Katika historia hapakuwa na chochote ila ardhi wazi. Wakati Hija hii ilipoainishwa, watu walikuwa wakirusha mawe sehemu hiyo pekee, kisha pakachimbwa shimo na nguzo ndogo ikatengenezwa, na sasa pametengenezwa ukuta hivyo basi ni jukumu la wanachuoni kuainisha ni sehemu gani ya ukuta inayohitaji kupigwa mawe. Hiki ni kitendo cha ishara ambapo kiuhalisia Shetani hayupo kwenye ukuta ule, bali Shetani huyo yupo ndani yako, yumo nyumbani, na katika jamii. Hii ilikuwa ni desturi ya Ibrahim ambayo imekua silabasi kwetu.

Qurbani maana yake ni kuwasilisha kila kitu unachokipenda mbele ya Mwenyezi Mungu ili uwe karibu na Mwenyezi Mungu. Jambo la tatu ambalo liko katika njia yako kuelekea kwa Mwenyezi Mungu, kama mke, watoto, mali, nyumba, mali, Unapaswa kuangalia kile unachopenda, Lazima ukague kutaka kujua ni nani unayempenda zaidi. Hii haimaanishi kwamba uwaache watoto wako au wake zako bali badala yake uyawache mapenzi yako na kuyafanya mapenzi hayo kuwa kwa Mwenyezi Mungu pekee.

Tunapaswa kuyakabidhi kwa Mwenyezi Mungu. Mke, Mume, watoto, njia ya maisha ni mahitaji yako. Hatujaambiwa tuchome kila kitu. Ilikuwa ni mapenzi ambayo yalitakiwa kutoka kwa Ibrahim kutoa dhabihu. Leo tunapaswa kutoa desturi hii ya dhabihu, lakini sio tu kutoa sadaka kila kitu unachofanya kwenye Hija kilikuwa kwa ajili ya ukaribu wa Mwenyezi Mungu.

Baadhi ya watu hawako tayari kunyoa vichwa vyao na ndio maana hawaendi kuhiji. Wakati huwezi kunyoa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu basi nini kingine unaweza kukifanya kwa ajili yake. Huna mapenzi na Allah hata kiasi hiki cha kunyoa kichwa basi unaweza kufanya lipi.

Tambiko hizi zote zina kiini kirefu ndani yake. Mwenyezi Mungu atupe Taufeeq tutembee katika nyayo za Ibrahim. Leo tuna furaha siku ya Idi kwa sababu tumefuata mtindo wa maisha wa Ibrahim na tumefanya agano hili leo kwamba tutaishi maisha ya aina hii.

 

Hotuba ya 2: Sherehe na Ubaidullah na Umar ibn Saad kwa ajili ya Uchaguzi

Tunapaswa kuitumia Taqwa katika maisha yetu, na kuifanya kuwa msingi wa mahusiano yetu yote, katika nia au maamuzi na katika mambo yote tunafaa tuifanye Taqwa kuwa sera ya yatu kwani mpango huu ni kwa ajili ya usalama wetu. Tunapaswa kupata faida kutoka kwenye Taqwa katika dunia hii nayo itatupa usalama wa maisha. Leo kwa kukosa Taqwa tunaiona hali ya Waislamu ilivyo.

Tumeiondoa kabisa Taqwa maishani. Dini yetu, serikali, siasa hazina Taqwa na maisha kama hayo yanakuwa ni yenye ghadhabu. Ingawa mataifa yote ya Kiislamu yanaishi maisha ya ghadhabu kama haya, lakini kwa Pakistani ni zaidi. Na hao hao wateule waliochaguliwa serikalini wamekuwa ghadhabu. Ghadhabu ya kidunia ni Khiz’y ambayo ni fedheha wanayoipata watu wanapotoka katika mfumo wa Allah na Quran na Ahlulbayt na kuwa wazinzi, walevi kama walivyoviongozi.

Qur’an imeamrisha ya kwamba tujitenge na watu kama hao na ndio mliowafanya Maimamu wenu na watakuwa ghadhabu juu yenu. Imam Ali (a) anasema kwamba umemuasi Imamu wako na wale watakaokuja kuchukua sehemu yake basi nao watakuwa ghadhabu juu yako. Ghadhabu iliyokuja kupitia kwa Banu Umayyah juu ya Waislamu ambapo madhalimu wengi wakishenzi waliwajia watu. Leo hii kile tunachokiita siasa ni ghadhabu ya kimungu. Tunaishi maisha ya ghadhabu ambayo tumeyanunua kwa mikono yetu wenyewe kwa kuiacha Taqwa.

Hali ya uchumi imefikia hali ya kufilisika na ni mbaya zaidi kuliko Sri Lanka. Tuna watu milioni 240, wanaoishi kwenye ardhi yenye rutuba na badala yake sisi tunalenga kuiharibu na hii ni ghadhabu. Kwa njia zote za maisha zilizopo tunanyimwa mahitaji ya maisha. Wale ambao tulikuwa tukiwaita watu weupe kuwa wanaishi maisha ya heshima; leo watu kama hao nao wanaomba.

Leo hivi rushwa imekuwa sheria nchini Pakistan na inabidi utoe hongo. Rushwa hiyo imekua ya kawaida kwa sababu wakati mahitaji ya maisha yasipotimizwa na ikawa wakati huo huo unayakuza maisha ya kimagharibi, wakati unapovutiwa na maisha ya anasa lakini ikawa njia za maisha hazipo basi watu watatimiza matamanio haya kwa kupitia rushwa. Huenda kusiwe na mtu yeyote ambaye hajatoa rushwa. Unaenda kutengeneza pasi ya kusafiria au kuchukua bili ya umeme, leseni ya kuendesha gari, kudahiliwa vyuoni na chochote unachotaka kufanya lazima ulipe na ziada.

Haramu hii ilikuja vipi katika uchumi wetu kwa sababu mahitaji ya watu yamekuwa mengi na kipato kimekuwa kidogo kwa hivyo itabidi itimizwe kwa njia ya Haramu. Mfumo umekuwa ukiendelea hivyo. Sasa hali ni kwamba hata Haram hii imekuwa haitoshi. Huwezi hata kununua nyanya, vitunguu, viungo kwakua havinunuliki. Huwezi kulipa ada ya shule kwa ajili ya watoto.

Wamewafungulia watu njia ya tatu. Ushuru umeongezwa, mfumuko wa bei umepanda na sasa watu wenye mizigo wana njia moja tu nayo ni uhalifu. Sasa watu hawatapokea rushwa lakini badala yake watafanya ujambazi na kwa ajili hiyo mauaji yataanza. Unapotazama habari za uhalifu. Habari za jana, mtoto wa kiume alimchinja babake mzazi huko mjini Wazirabad kwenye soko la wazi.

Haya yanatokea kila siku. Katika gazeti hilohilo zikaja habari kuwa shemeji amemuua mkewe na shemeji yake kwa ajili ya masuala ya mirathi. Kwa mtazamo wetu ni kuwa hawa ni waathirika wa dawa za kulevya wanaofanya vitendo kama hivi lakini ukweli unatokana na siasa zisizo na Taqwa ndio chanzo cha haya yote. Walio na hatamu za serikali mikononi mwao wameifikisha nchi katika hali hii.

Ikiwa nyumba ya mtu itakua katika hali nzuri ya kimaisha lakini  jirani yake awe kwenye shida. Hatimaye wanakuja kujua kwamba mtu katika nyumba hii ni dacoit (mwenye kuhitaji zaidi) kuwaliko wao pia na kudai kuwa sehemu ya baadhi ya genge.

Baada ya Eid, kutakuwa na uchaguzi ambapo kila kitu kitatumwa kwa ghadhabu hii ya uchaguzi. Kama taifa hili lingekuwa na akili walipaswa kuwarushia viatu wagombea hawa wanaotaka kura. Chama kimoja kilitawala kwa miaka minne kama ghadhabu na chama kingine pia kimefanya vibaya zaidi baada yao.

Sasa pande zote mbili zimekuja na wafuasi wa Karbala, Imamu Husein. Kwa sasa mashindano ni kati ya Umar Ibn Ziad na Ubaidullah. Je, hii ni Taqwa, akili na elimu? Mnapaswa kuwa mumejitenga na haya yote.

Waambieni kwamba sisi tunakupinga na ni maadui kwako. Wameibadilisha Taghot na kuifanya kuwa ghadhabu kwa watu. Uliitwa kuhiji  umpige mawe Shetani huyu wa kisiasa na ukapewa wokovu.

Mfano huu wa kuigwa kutoka kwa Nabii Ibrahim ulikuwa kwa ajili ya hili. Mtume amesema, aina 3 za hija zitafanyika, zingine kwa ajili ya biashara, zingine kwa ajili ya anasa na baadhi ajili ya kupata umaarufu. Watapiga picha za selfie kutoka kwenye mnara wa Mecca ulio mita 100 juu ya Kaaba kama matusi na kebehi.

Umefanya Hija ya Kizayuni na sio Arafa. Mwaka huu khutba iliyofanyika Arafa tarehe 9 Dhulhijja ilitolewa na mzungumzaji wa Kizayuni. Hii ni kwa sababu Biden anakuja na jopo la kushawishi la Wazayuni hadi Madina. Wanataka kufanya mapatano ya Ibrahimi. Kwanza ulikuwa umekaa kimya juu ya Baitul Muqaddas na sasa unaiokoa Haramain yako kutoka kwa hawa Wazayuni, waliokuwa wakidai kuwa sisi ni watetezi wa Haramain. Wameiweka Haramain jina la anasa huko ambalo wanataka kutetea.

Mfano wa kuigwa wa Ibrahim ndio njia ya wokovu. Taifa linapaswa kutangaza kujitenga na watawala hawa. Mkiwa miongoni mwao, na mkawaunga mkono, Mwenyezi Mungu anasema msiwe pamoja na wafuasi wa madhalimu. Imam sajjad katika Dua e Arafa anasema usinifanye kuwa mfuasi wa madhalimu na watawala jeuri.

Hili ni jukumu la kielelezo cha Ibrahim (a)na hivi sasa ndio wakati wa  kuchukua hatua juu ya swala hili nchini Pakistan. Ummah huu unapaswa kupata njia iliyonyooka ya Ibrahim ambayo haiendi kushoto wala kulia.

Unataka kumuacha Imamu Husein (a) na kusema Labbaik kwa Umar ibn Sa’ad. Kama vile kule mjini Kufa ulipomwalika Imam Husein (a) na sasa umesimama pamoja na jeshi la Umar ibn Saad. Je, hizi Azadar za Husein haziwezi kukomesha uhalifu huu.

Umetengeneza burudani hii kuwa nani anaenda na nani? Kwa nini unakuwa sehemu ya ghadhabu. Hutapata hata mifupa kutoka kwao, hakuna utakachopata na bado unaenda kwa miguu yao na kisha kutoa uhalali.

Huyu ndiye kiongozi cha Ibrahim (a)? Tunamuomba Mwenyezi Mungu katika siku hii kuu ailinde Pakistan, alipe wokovu taifa hili kutokana na watawala, alipe akili na mwamko taifa hili, awafedheheshe maadui wa ndani na wa nje wa taifa hili, atujaalie kuwa viigizo vya Nabii Ibrahim (a) na  Imam Husein (a).

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *