Hapo jana waandamanaji wa Israel walifunga moja ya barabara kuu za mji wa Tel Aviv kuelekea kaskazini na kukusanyika mbele ya nyumba ya Spika wa Bunge la Knesset na Waziri wa Sheria wa utawala huo ghasibu wa Kizayuni.
Walowezi hao wa Kizayuni waliingia mitaani katika wiki ya 32 ya maandamano dhidi ya sera za baraza la mawaziri la Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu hususan kile kinachoitwa sheria ya mabadiliko ya mahakama.
Vyombo vya habari vya Kizayuni vimeripoti kuwa waandamanaji walifunga barabara kuu ya Elon inayoelekea kaskazini karibu na Tel Aviv.
Waandamanaji pia waliketi mbele ya nyumba ya Spika wa Bunge la Knesset na Waziri wa Sheria wa utawala wa Kizayuni huko Tel Aviv.
Msururu wa maandamano dhidi ya Netanyahu na sera zake za baraza la mawaziri uliokithiri unazidi kuongezeka kila wiki na kujumuisha Wazayuni wengi zaidi kutoka vyama na sekta tofauti. Wapinzani wa Netanyahu, ambao wanajumuisha idadi kubwa ya Wazayuni, wanauita mpango wake wa kubadilisha sheria za mahakama kuwa ni mapinduzi ya kimahakama.
Waandamanaji wa Kizayuni wanauchukulia mpango huu wa baraza la mawaziri la Netanyahu kusababisha machafuko na wanaamini kuwa kwa kutekeleza mpango huo, Netanyahu ataweza kufanya lolote bila ya usimamizi wa Mahakama ya Juu.