Kuzuiliwa kwa Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi

Vikosi vya utawala dhalimu vilivamia maeneo mbalimbali ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na kuwatia mbaroni baadhi ya raia.

Kwa mujibu wa idhaa ya kimataifa ya Shirika la Habari la Fars, vikosi vya utawala wa Kizayuni vilishambulia maeneo tofauti ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan asubuhi ya leo na kuwatia mbaroni raia kadhaa wa Palestina.

Vyanzo vya habari vya Palestina vimeripoti kuwa wanajeshi wa Israel waliwaweka kizuizini raia wanne huko Hebroni na Bethlehem.

Vilevile waliwakamata wawili kati ya waliokua wafungwa hapo mwanzoni, miongoni mwao Sufyan Jamjum aliyekua kwake nyumbani huko al-Hawwaz na Ja’far al-Qawasemi kutoka kwake nyumbani iliyopo katika maeneo ya Wadi Abu Aktila mjini Hebron.

Kwa mujibu wa tovuti ya Arab 48, vikosi vya Israel pia vimewazuilia Wapalestina kadhaa katika kambi ya Aida huko Bethlehem.

Katika Ukanda wa Gaza, vikosi vya utawala dhaimu vilifyatua risasi katika ardhi ya kilimo mashariki mwa mji wa Abbas katika jimbo la Khan Yunis.

Raia wa Kipalestina walisema wanajeshi wanaoikalia kwa mabavu walioko katika mnara wa kijeshi mashariki mwa eneo la al-Sunnati walirusha makombora mazito ya mizinga katika mashamba ya Wapalestina. Pia walianza kufyatua risasi mashariki mwa Balad al-Fakhari huko Khan Yunis, na kusababisha hofu miongoni mwa raia, haswa watoto na wanawake.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *