Mlipuko mkubwa wa ugonjwa wa omicron bado unaendelea katika baadhi ya majimbo ya China, huku idadi ya wahasiriwa wa corona nchini ikifikia 4,638, kulingana na takwimu zilizorekodiwa.
Kulingana na Shirika la Habari la Associated Press, maafisa wa afya wa kitaifa wa China mnamo siku ya Jumamosi waliripoti vifo viwili vilivyotokana na virusi vya Covid-19, ikiwa ni ongezeko la kwanza la idadi ya vifo tangu Januari 2021, huku nchi ikipambana na ongezeko la wa omicrone.
Idadi ya waliofariki, iliyorekodiwa kaskazini mashariki mwa Mkoa wa Jilin nchini China, ilifikia kiwango cha 4,638. Uchina iliripoti kesi mpya zilizofikia idadi ya 2,157 za Covid-19 siku ya Jumamosi, nyingi zikiwa zimesajiliwa kutoka Jilin. Jimbo hilo limeweka marufuku ya kusafiri, na watu watahitaji vibali vya polisi wakati wa kuvuka mipaka.
Tangu kuzuka kwake kwa mara ya kwanza huko nchini Wuhan, Uchina imeendelea kutumia mikakati yenye mafanikio, ingawa ni hatua ngumu na yenye gharama kubwa. Mkakati huo unaangazia majaribio makubwa na karantini kali huku wakaazi wakikumbana na marufuku ya kuondoka nyumbani kwao hadi vitu vyote vipya vipatikane katika karantini au kufuatiliwa.
Huku Uchina sasa inakabiliwa na mlipuko wake mbaya zaidi tangu mwishoni mwa 2019, maafisa wameahidi kuongeza mkakati kamili wa sifuri ili kupunguza ongezeko la sasa.
Walakini, kiongozi wa Uchina Xi Jinping mnamo Alhamisi kwa mara ya kwanza alikubali matokeo ya hatua hizo, akisema China inapaswa kutafuta “athari ya juu” kwa “gharama ya chini” katika kudhibiti virusi.