Kwa mara ya tisa, bunge la Lebanon lashindwa kumchagua rais mpya

Jaribio la tisa la Bunge la Lebanon kumchagua rais mpya wa nchi hiyo limegonga mwamba.

Hadi sasa, vimeshafanyika vikao vinane vya bunge la Lebanon kwa lengo la kumchagua rais mpya wa nchi hiyo lakini hakuna tija iliyopatikana.
Katika kikao kingine walichofanya jana Alkhamisi, wabunge wa Lebanon walishindwa kwa mara ya tisa kumchagua rais mpya wa nchi hiyo.
Katika mkutano wa jana wa bunge la Lebanon, hakuna mgombea hata mmoja aliyeweza kupata thuluthi mbili ya kura za wabunge wa bunge hilo.
Mkutano ujao wa bunge la Lebanon kumchagua rais mpya utafanyika Alkhamisi ijayo.
Kabla ya hapo, maafisa wa harakati ya Hizbullah walishatahadharisha mara kadhaa kuhusu njama za ubalozi wa Marekani na vibaraka wake za kuzusha mpasuko kati ya Walebanon katika uchaguzi wa bunge la nchi hiyo.
Sheikh Nabil Qawouq, mjumbe wa Baraza Kuu la Harakati ya Hizbullah amebainisha kuwa, si siri tena kwa Walebanon kwamba ubalozi wa Saudi Arabia nchini Lebanon unaingilia uchaguzi wa rais kama ulivyoingilia uchaguzi wa bunge, lakini uingiliaji wa mara hii ni wa moja kwa moja na usio na kiunganishi, mpaka imefika hadi baadhi ya wabunge wanalalamika kwamba wamekuwa wakikabiliwa na mashinikizo kutoka balozi za Marekani na Saudi Arabia nchini humo.
Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *