Kwa Nini Uadilifu Ni Muhimu Kama Msingi Katika Jamii Ya Wanadamu? Hujjatul Islam Ustad Syed Jawad Naqvi

Hujjatul Islam Ustad Syed Jawad Naqvi
(Principal Jamia Orwatul Wuthqa – Lahore)

Delivered at: Masjid Baitul ul Ateeq
Lahore – Pakistan

Hotuba ya ijumaa – 8th March, 2024

 

 

Hotuba ya 1: Kwa Nini Uadilifu Ni Muhimu Kama Msingi Katika Jamii Ya Wanadamu?

Hotuba ya 2: kuimarisha nguvu ya utashi  (Iraada) – ni muhimu kwa Ramadhan

Mpango wa Taqwa una muundo na uadilifu ndio msingi wake. Kwa kuwa mfumo wa kiungu unategemea uadilifu basi uadilifu ndio msingi wa maisha ya mwanadamu, jamii na dini pia. Allah aliwatuma mitume wakiwa na uongofu ulio wa wazi, kitabu, mzani na kwa mujibu wa Aya ya 25 ya Suratul Hadid chuma pia kimetumwa ambacho kina ugumu ndani yake. Imamat ndio nafasi pekee ambayo imepewa majukumu ya kusimamisha uadilifu. Imam huchaguliwa na Allah kwa mujibu wa vigezo alivyo viweka Allah mwenyewe.

Kwanini uadilifu ni muhimu kama msingi katika maisha ya jamii ya mwanadamu? Ili kuelewa hadhi ya uadilifu tunahitaji kufanya majadiliano ya kifalsafa. Katika kuunda uadilifu tunahitaji kujadili kunako utambuzi wa mwanadamu. Na kwa ajili ya uadilifu katika uwepo, na katika sifa za Allah tunahitaji majadiliano ya kidini na hivyo hivyo kwa jamii ya mwanadamu tunahitaji sayansi ya kijamii. Kwa Upande wa Qur’an imekuja Aya ya 25 ya Suratul Hadid na Aya nyinginezo. Kwanini jamii ya mwanadamu inatakiwa kuanzishwa kwa msingi wa uadilifu na kwanini jamii inatakiwa kutathminiwa kwa kipimo cha uadilifu juu ya kujua ina thamani kiasi gani.

Imamu Ja’far Sadiq ( a.s) ametaja umuhimu wa uadilifu katika jamii ya mwanadamu. Hadithi hii ipo ndani ya Tahful ‘Uquul. Uadilifu ni hitajio la kila binadamu na sio tu kwa Imani Fulani. Kwa mu7jhibu wa hadithi hii imam Sadiq ( a.s) anasema kuna mambo matatu ambayo wanadamu wote wanayahitaji: kwanza ni Amani, Uadilifu na Khisb ( ustawi katika maisha ya dunia)

Uadilifu ni uaswa ambao husimamishwa sehemu zote kama kiwango na mfumo wa Allah. Khisb ina maana ya ustawi na faraja katika maisha ambapo nyenzo zake ni, ni kwamba mambo yote muhimu ya maisha  yanatakiwa kuwa wigo mpana na sio kubanwa. Moja ya mahitaji muhimu katika maisha ni nyumba ambayo inatakiwa ukubwa wake uzingatie idadi ya watu watakaoishi katika nyumba hiyo. Haitakuwa Khisb ikiwa kutakuwa kuna watu kumi wanaishi katika chumba kimoja. Hitajio muhimu la pili ni chakula ambacho ni hitajio muhimu tokea kuzaliwa hadi kufa ili kuweza kusihi na kuwa na afya. Hitajio hili inabidi liwepo kwa kiasi kikubwa kwa ajili ya wanafamilia wote. Kisha mavazi ambalo ni hitajio lingine ambalo inabidi mtu alipate kwa mahitaji ya hali ya hewa tofauti tofauti n.k. Na kuna mahitaji mengine ambayo mtu anatakiwa kuwa nayo ndani ya nyumba. Mtu anatakiwa kuwa na usafiri ambao unaendana na mazingira na zama anazoishi kama ilivyokuwa katika zama zilizopita walikuwa wakitumia punda, ngamia, na nyumbu na katika zama zetu hizi za sasa aina ya usafiri inayohitajika inabidi kuwa nayo. Na kwa ajili ya maradhi yake inabidi dawa inabidi ziwepo. Nyenzo hizi hizi zote inabidi ziwepo ili kuleta faraja katika maisha ya mwanadamu. Hii havitakiwi kuwa kwamba mwanadamu atumie maisha yake yote akitafuta nyenzo hizi. Maisha ni yenye thamani zaidi ambayo hayajakuwepo kwa ajili ya kutafuta nyenzo hizi. Hiki ndicho kinachotokea na huenda kitatokea baadaye pia kwamba mwanadamu kutumia maisha yake yote kwa ajili yakupata nyenzo hizi za maisha. Hizi nyenzo zinatafutwa kwa ajili ya maisha na maisha husimamishwa kupitia nyenzo hizi ili kupiga hatua ya kulielekea lengo la kuumbwa. Lengo la kuumbwa sio nyenzo. Ustawi huu ndio hitajio la wanadamu. Katika mtaala wa masomo yetu ya dini tunapofundishwa kwamba sehemu kubwa ya dini yetu ni maadili pamoja na upande wa kijamii kwa mtazamo wa kidini na siasa iliondolewa kutoka kwenye dini tangia siku ya kwanza. Wasomi na maulama waliweka maadili kuwa ndio dini na upande mwingine ikiwa ni ibada. Haya mambo ndio yamekuwa yakifundishwa kama dini kwa karne nyingi. Waliondoa upande wa dini wa kijamii kwanza na kisha ikaondolewa siasa. Katika maadili na ibada mambo matatu haya ambayo aliyataja imamu Sadiq(a.s) hayatakiwi. Amani na Uadilifu mambo haya hayapo kwenye maadili. Kiongozi wa kidini anasema mambo matatu ni mahitajio ya kila mwanadamu. Ikiwa tutachunguza mtaala wa masomo ya dini tunaona kwamba maisha bora yanakemewa sana. Wanasema yanaweka mbali watu na Allah na wameyapa jina la kimaada na hayaendani na kiini cha ibada. Pindi utajiri unapokuja basi kuna rushwa na ikiwa utakuwa ni mwenye kupenda mali hata kwa kiasi kidogo basi utakuweka mbali na Allah tumefunzwa haya kutokana na hisia za dini. Katika mchakato huu mambo mengine mengi ya uhakika na uhalisia yameondolewa na kubakishwa maadili ambayo yanatangazwa kwa jina la dini. Ikiwa mtu atakuwa tajiri basi kila mtu hufikiri kuwa ni fisadi. Hivi ndivyo picha ya dini inavyowasilishwa tofauti ambayo imeacha matokeo mabaya kwa dini.

Imam Khomeini (r.a) anasema dini inawasilishwa na mifumo mitatu; mfumo wa kwanza ni Uislamu asili ambao upo kama alivyo uteremsha Allah ambao hakuna marekebisho na mabadiliko ndani yake kutokana na mikono ya mwanadamu. Mfumo wa pili ni wa Thajjur ambao una maana ya kuwa na akili finyu. Katika dini hii asili na msingi wa dini vimeondolewa na kwa mtazamo wa Iqbal anasema kilichobaki kwenye dini ni ibada tu, mila na baadhi ya maadili. Upande wa kijamii na kisiasa vimeondolewa kutoka kwenye dini kabisa. Dini ambayo inakidhi mahitaji ya binadamu ndiyo dini kamili na ndivyo Allah aliyotufundisha na ndivyo inavyotakiwa kufikishwa kama ulivyo. Kisha jamii huundwa kama alivyoagiza Allah. Mfumo wa tatu wa dini ni umetajwa na Imam ni dinul i’itiqad  ( dini iliyo chafuliwa) katika dini kuna mambo ya nje ya dini yameongezwa. Mila, Bidaa, upotoshaji, ukorofi, mifumo isiyokuwa ya kidini ka ma demokrasia vimeongezwa katika dini. Kisha haya yalifanyiwa matangazo na kuhubiriwa na sisi tunayafuata kwa nguvu zote haya mambo yaliyo chafuliwa na haturuhusu yaondolewe. Mifumo hii mitatu ya dini ipo sehemu zote. Kutokana na uchafuzi katika dini, Qur’an kisha madhehebu ndio yamekuja. Uislamu sahihi ni Qur’an na ndio alio uwasilisha Mtume Mtukufu.

Imam Sadiq (a.s) anasema dini inawasilisha mambo matatu muhimu kwa binadamu. Imam Sadiq (a) anaelezea na kufafanua dini. Hitajio la kwanza ni Amn , Adl na Khisb. Sasahivi kama utaangalia maadili ndani ya dini basi khisb ( maisha bora) ni yenye kuhukumiwa vibaya na wanataka muumini awe ni mwenye njaa siku zote. Bila ya maisha ya starehe mwanadamu hawezi kupiga hatua mbele. Namna gani nyenzo za maisha zitamfikia mtu? Mtu anatakiwa awe na nyenzo za maisha na asiwe tegemezi naombaomba kwa wengine. Khisb inatajwa kuwa ni ibada kubwa. Katika mafunzo yetu ya kidini kuchuma mali hakuitwi kuwa dini bali wanaochuma mali huzingatiwa kuwa ni watu wa kidunia. Kisha mfumo wa uadilifu hautajwi kwenye katika maadili yetu na ibada. Kilele cha uadilifu ambacho hutajwa kwenye ibada ni kwamba imamu wa jamaa anatakiwa kuwa muadilifu, sasa je vipi kuhusu wale wanaosali nyuma yake ( maamuma)? Hawatakiwi kuwa waadilifu. Kila mtu mwanaume , mwanamke, msomi na wanajamii wote wanatakiwa kuwa waadilifu. Dini imefanya uadilifu kuwa ni jambo muhimu sana kwa ubinadamu. Hivyo basi amani ni hitajio la kiulimwengu ambalo kila mtu anaihitajia.

Haya yote yanahitajika kwa ajili ya utafutaji wa mwanadamu kufikia lengo la maisha. Haya mambo matatu huandaa mazingira na njia ambayo mtu anaitumia kufikia malengo yake. Ni kama mmea ambao inabidi ukue na kutoa matunda. Utaweza fanya hivyo pindi kutakapokuwepo udongo sahihi, hewa, maji na mwanga. Uadilifu huandaa mazingira ya maendeleo ya mtu. Amn ni huo udongo ambapo mwanadamu hupata fursa ya kujifunza na kukua. Kwa mujibu wa waislamu walio wengi usalama umechukuliwa kutoka kwa mtu. Panapokosekana usalama basi huwezi kufanikiwa kuyafikia malengo yoyote ya maisha. Kwa ajili ya kuwa na mazingira salama ambapo kuna Amn basi mnahitaji uadilifu. Kama hakuna usawa katika jamii katika upande wa kiuchumi, siasa n.k. na ikiwa watu stahiki hawapo kwenye nafasi zao sahihi basi hii itakuwa ni jamii isiyokuwa na usawa. Katika jamii hii hakuna mazingira ya mwanadamu kukua kiasili. Kutokuwa na usalama, kutokuwepo usawa na kubanwa nyenzo za maisha hupelekea jamii kushindwa kulea wanadamu. Popote pale tutakapoona katika jamii na kujiuliza kwanini mwanadamu hakuna thamani , hakuna ubinadamu , watu ni mafisadi, kwanini hakuna subira, busara na hisia kwa watu. Wanahamasika na kusisimkwa wanapoona maandishi ya Kiarabu yakiwa yameandikwa sehemu na kudhani kuwa ni maneno ya Qur’an. Kama utawatazama wanadini utawakuta ni watu wenye misimamo mikali, fikira finyu, kisha ukitazama wanasiasa unakuta wapo vibaya zaidi, unatazama wafanya biashara unakuta wamejaa uchu na tamaa na wazalishaji wanafanya uchafu na uchakachuzi. Kwanini jamii nzima inasumbuka? Kwanini watu wa sawa na shakhsiya kubwa hawazaliwi. Kimsingi na mzizi wake ni kwa sababu ya kutokuwepo mambo hayo matatu ambayo ni Amn, Adl na kupata nyenzo za kuishi maisha bora. Hii ni jamii ya aina gani ambayo kuna wenye tamaa, njaa ya madaraka, misimamo mikali, Takfiri na wavunja amani wanapata nguvu mahala ambapo ushwa na ufisadi umeenea kila sehemu. Hata mila na ibada zinapofanywa na unaweza kuona maandalizi. Baada ya Ramadhani kuisha hakutakuwa utoaji hata mmoja utakaokua kwa sababu msingi wa jamii unategemea Amn, Adl na Khisb. Kiashiria cha msingi ni uadilifu ambapo mtu kupitia kwacho huifikia ubinadamu na huu uadilifu umetelekezwa na kutolewa katika mitaala ya masomo yetu dini. Kwanza tuliondoa kipengele cha jamii na siasa na kumkabidhi Taghuti. Leo tunataraji kuwa Ahlul Bayt na maswahaba zao kwamba wapo baina yetu. Jamii ambayo msingi wake umeegemea katiika mafunzo kutoka kwa Ahlul Bayt ndio wanaoweza tu kulea watu wa namna hii. Kuishi na makundi ya Banu Umayyah  huwezi kutaraji kuwa binadamu.

Tangu vita ya Gaza ianze, nilitaja tangu awali ya kwamba tunaweza kuelewa kwamba Israel, na Amerika wanafanya ushenzi, lakini kwanini watu wote wapo kimya? Je hii ni kwa sababu ubinadamu wao sio wenye kukua. Unaweza kuona katika nchi yako ambapo wanadai kuwa ni wengi kwenye dini lakini hakuna ubinadamu hata kwa mbali. Dini pasina ubinadamu ni udanganyifu. Hivyo, uadilifu ni msingi wa kumlea mwanadamu. Uadilifu ni msingi wa kila kitu. Tunamuomba Allah atupe ufahamu wa dini asili na sahihi na mfumo wa Taqwa.

Hotuba ya 2

Mwezi mtukufu wa Ramadhani ni mwezi muhimu sana kwa ajili ya kupata Taqwa ambao tunauingia sasahivi. Mtume Mtukufu (s.a.w)amesema: umekuelekeeni mwezi wa Allah na nyinyi mnatakiwa kuupokea na kuukaribisha na kuweni tayari kwa ajili ya Ramadhani. Mambo ambayo mtu hawezi kuyafanya katika miezi kumi na moja vinakuwa rahisi kwa mtu kuvifanya. Uwezeshwaji huu pia hutoka ndani. Mtu hujiandaa mwenyewe kwa ajili ya kufikia malengo haya. Mwezi wa Ramadhani ni warsha ya imani. Katika warsha hii Allah ameweka adabu fulani na kumuandalia mazingira mwanadamu. Vikwazo vinaondolewa na ni fursa ambayo unapaswa kushukuru.

Kuna kuchanganya ambako kunatokea katika ibada. Kila ibada ina tabaka tatu. Ya kwanza ni upande wa nje au mila. Ya pili ni ndani ambayo ina maana ya kiroho. Tatu n siri ya ibada. Mambo haya matatu yapo katika kila mfumo wa ibada. Tumeweza kutafsiri ibada fulani za Qur’an lakini kuna baadhi kama zakat hazijatafsiriwa na tunashukuru kwamba zakat na Hajj hazijatafsiriwa. Lakini Sala na Saumu zimetafsiriwa. Sala imetafsiriwa kama maombi na Saumu kama kufunga . tumetafsiri saumu kama kubaki na njaa. Katika Sala inasemwa kwamba inabidi uitekeleze ukiwa na uwepo wa moyo lakini kivipi? Watu huwafuata maulama wetu wanaotufundisha na ya kuwa makini na mazingatio ndani ya Sala na mtu bado hubaki akiwa na wasiwasi kuhusu hili. Ni ngumu sana kwa watu wengi kutuliza akili na kuwana mazingatio katika sala. Ikiwa tutazingatia upande wa nje wa sala na tukakidhi matakwa yake. Utakuwa unategemewa kuleta uwepo wa mwili ambao unawasilishwa kwenye sala ukiwa na kuchunga adabu zake. Ikiwa utafanya hizi basi utakuwa umesimamisha sala yote kwa ujumla. Sisi tunanyimwa kutoka kwenye tabaka la kwanza la nje ambalo ni la mwili wenyewe. Hivyo hivyo Saumu pia ina upande wake wa nje ambao unafikiwa na kila mtu. Wale ambao hawawezi kufikia kiini cha uwepo wa ndani wenyewe wanawakatisha tamaa wengine kwa kuwaambia kuwa sala zenu hazina faida. Hata kama utakuwa hujafikia tabaka la ndani la sala lakini bado ujue kwamba Allah anakutaka ukamilishe hatua ya kwanza ya uwepo wako wa upande wa nje.

Hali hii pia inafanya kazi katika mwezi wa Ramadhani pia, ambapo unatakiwa kuhakikisha uwepo wa nje, kisha baada hatua hii hatua inayofuata itakuwa rahisi. Katikia mwezi wa Ramadhani unatakiwa kuukuza upande wa nje inavyotakiwa. Kitu cha msingi kinachotakiwa katika mwezi wa Ramadhani ni nia au utashi ( irada). Mwenyezi Mungu humpa mwanadamu huyu tabia endelevu. Tunaishi kwa tabia na sio kwa nia. Tunakula na kunywa kwa kufuata tabia. Tunakula katika muda maalumu kwa tabia. Hii sio nzuri kwa mtu kwamba anakuza tabia kwanza kisha baadaye anakuwa mateka wa tabia. Hivyo Ramadhani imeletwa kwa ajili ya kumkomboa mwanadamu kutokana na umateka wa mazoea ya kitabia. Irada au utashi na tabia siku zote ni maadui. Kwa kadri utashi utakavyokuwa na nguvu ndivyo tabia itadhoofika na kinyume chake ni hivyo pia. Hatuwezi kubadili tabia au mazoea kwa sababu nguvu ya utashi wetu ni dhaifu. Hii ni neema kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwamba ametupa mwezi wa Ramadhani. Ni mwezi unaokuja na neema tele. Mtume (s.a.w) anasema kwamba mwenyeji anakuja na kila kitu kwa ajili yenu na nyinyi basi mnatakiwa kupokea kwa kuwa ni wageni. Nje,  huu ni mwezi uliojaa baraka. Inabidi uingie ndani ya mwezi wa Ramadhani ukiwa na maandalizi. Miezi ya Rajabu na Shaban imewekwa kwa ajili ya kufanya maandalizi. Pindi mwanadamu anapokuwa huru katika mwezi huu basi fadhila na riziki za Allah huongezeka.

Katika mwezi huu wa Ramadhani, tunatakiwa kuacha tabia binafsi na tabia baadhi za kijamii, tuzipe nguvu tabia zetu, tusafishe nguvu zetu za utashi na tuzifanye kuwa ni zenye kuendana na matakwa ya Allah. Nitafanya kila kiu ambacho ndani yake anakusudiwa Allah. Hili linawezekana ndani ya mwezi wa Ramadhani. Moja ya jambo muhimu ambalo huja ndani ya Ramadhani katika kumi la mwisho. Mtua baada ya siku ishirini anakuwa  kawa huru hivyo basi unatakiwa upaza sauti yako kwa ajili ya watu wanaodhulumiwa. Mwaka huu sisi sote tunajua nini kinaendelea kutokea. Tumeshachelewa, watu wengi wameshauliwa huko Gaza na idadi ya majeruhi ipo juu sana. Kuna kupigwa mabomu kwa kila siku na tangia siku chache zilizopita dhuluma inayoendelea ni pale ambapo watu wenye njaa, kiu na majeraha wanaposimama kwa ajili ya kupata chakula kuna mashambulio ya mabomu yanafanyika na kuwaua kishahidi. Mchezo huu umeendelea kushuhudiwa na watu wote. Hivi ni kwa sababu hawana ubinadamu na ili kuamsha ubinadamu Allah kauweka ubinadamu.

Maimamu wanasema kwamba kuna njaa na kiu katika mwezi mtukufu ili kuweza kuamsha hisia zako zilizokufa. Hisia hizi inabidi ziamshwe ndani mwetu. Kila mtu ametwaa kosa la ukimya. Dhuluma ilianza tarehe 8 oktoba na sasa imefika 8 march na bado watu wapo kimya. Inataki9wa tumuombe Allah afufue ubinadamu wetu na maadili ambavyo vimezikwa chini ya tamaa. Pindi maadili haya yatakavyo fufuliwa kisha matakwa ya Mwenyezi Mungu, tutamaliza dhuluma katika dunia na tutaanza na Gaza. Maisha ya namna hii hayapendwi na dini, Mtume, Imam ‘Ali na Hussain. Kauli ya imam Hussain ( a) aliposema nazingatia kifo kuwa ni heshima na kluishi na madhalimu ni aibu na ni fedheha. Ni aibu kubwa kwamba waislamu wengi wanauliwa mbele ya macho yetu na hatupo tayari kupaza sauti zetu. Tumeshughulishwa na PSL cricket, umadhehebu na siasa. Wanasiasa wetu wana njaa ya madaraka na maulama wanaomba mgao wao katika siasa. Wengine wameshughulishwa zaidi na umadhehebu. Kwanza mashia waliuliwa na sasahivi Gaza imewekwa kwa mtazamo wa kimadhehebu. Wanasema kwamba Mashia wanasaidia Gaza ili kuwafanya watu kuwa mashia, hivyo basi Mashia wanatakiwa kumalizwa ndani ya Pakistan kwa sababu ni tishio. Huu ni uovu mnao ueneza. Walahidi wa USA, Uingereza na hata Mayahudi wanapaza sauti kwa ajili ya Gaza. Ni jambo la ubinadamu na Uislamu. Ibada kubwa zaidi leo ni kuwasaidia wanaodhulumiwa. Minong’ono ya kishetani kama hiyo haitakiwi kuzingatiwa. Hili linafanyika kwa malengo mengine. Watu wa namna hii ni wale wasiokuwa na jina sasa wanafanya haya ili kupata umaarufu. Inabidi tuufanye mwezi mzima wa Ramadhani kuwa ni Quds katika media, Sala, Ibada na inabidi tuwaombee hawa wanaodhulumiwa ili wapate unafuu. Mwenyezi Mungu na awaangamize madhalimu hawa na dhuluma yao.

Katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani mtu anatakiwa kujisafisha nafsi yake na maisha yake kupitia saumu. Waumini wote wanatakiwa kutoa zaka na khums ndani ya mwezi huu. Inatakiwa ujisafishe maisha yako yote katika mwezi huu na ujisafishe nafsi yako kwa kuwaunga mkono wanaodhulumiwa. Omba msamaha kutoka kwa Allah na waombee mashahidi.

 

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *