‘Lengo la Marekani la kuivamia Afghanistan lilikuwa ni kuzidhibiti nchi jirani’

Balozi wa Iran mjini Kabul Afghanistan amesema kuwa, lengo kuu la Marekani la kuivamia na kuikalia kwa mabavu Afghanistan halikuwa kupambana na ugaidi bali lilikuwa ni kuzidhibiti nchi zinazopakana na Afghanistan.

Shirika la habari la IRIB limemnukuu Hasan Kazeni Qomi akisema hayo katika mahojiano na televisheni ya al Alam na kuongeza kuwa, Wamarekani waliivamia na kuikalia kwa mabavu Afghanistan kwa madai na kisingizio cha kupambana na ugaidi, lakini lengo lao kuu lilikuwa ni kuzidhibiti nchi jirani na Afghanistan na kuyatia nguvu magenge ya kigaidi ya Daesh (ISIS) na al Qaida ambayo yanaendesha vita na yanafanyaa jinai na ukatili katika nchi za Waislamu kwa niaba ya Marekani.

Balozi huyo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Afghanistan ameongeza kuwa, hadi leo hii Wamarekani wanafuatilia siasa zao za kibeberu nchini Afghanistan ikiwa ni pamoja na kuwa na ushawishi wa kijeshi nchini humo huku mitandao ya kigaidi kama al Qaida na Daesh yakiendelea kuvuruga usalama wa nchi za Waislamu, kufanya mauaji na ukatili wa kila namna kwa niaba ya madola ya kibeberu hasa Marekani na kwa shabaha na kuipaka matope dini tukufu ya Kiislamu.

Ameongeza kuwa, Marekani inayatumia magenge hayo ya ukufurishaji kupigana kwa niaba yake kwa ajili ya kufanikisha malengo yake ya kibeberu, si Afghanistan tu, bali pia katika ukanda huu mzima.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *