Maandamano makubwa nchini Uswisi kulalamikia mshahara mdogo na ugumu wa maisha

Maandamano makubwa yamefanyika katika mji wa Lausanne nchini Uswisi kulalamikia kiwango cha chini cha mishahara, ugumu wa maisha na kupanda bei za bidhaa ambako hakuendani na mshahara wa wafanyakazi.

Kwa mujibu wa shirika la habari la IRIB, maelfu ya raia wa Uswisi walifanya maandamano makubwa Jumatatu usiku katika mji wa Lausanne, wakitaka nyongeza ya mishahara itakayoendana na kiwango halisi ya mfumuko wa bei na kupanda gharama za maisha katika nchi hiyo ya Ulaya.

Waandamanaji katika mji huo wa wa Uswizi wa Lausanne wa nchi ya Ulaya ya Uswisi wamepaza sauti zao kuungana na maandamano kama hayo katika nchi nyingine za barani Ulaya kulalamikia ugumu wa maisha, mfumuko wa bei za bidhaa na mishahara  midogo isiyoendana na hali halisi ilivyo.

Raia wa Uswisi, haswa wafanyikazi, wanalalamika kuwa uwezo wa manunuzi ya bidhaa unazidi kuporomoka, bei za bidhaa zinazidi kupanda, lakini mishahara yao haiongezwi.

Waandamanaji wa Uswisi pia wamelalamika kuwa, kiwango cha mfumuko wa bei kilichotangazwa na serikali ya nchi hiyo yaani asilimia 3.5 si cha kweli bali kiwango halisi cha mfumuko wa bei kimepindukia asilimia 5, hivyo wanataka nyongeza ya asilimia isiyopungua tano ya mishahara yao.

Hii ni katika hali ambayo, bei ya baadhi ya bidhaa, hasa chakula nchini Uswisi, imeongezeka kwa zaidi ya asilimia 15 tangu mwaka jana.

Wiki chache zilizopita pia kulifanyika maandamano mengine kama hayo nchini Uswisi na kama viongozi wa nchi hiyo ya Ulaya hawatosikiliza madai ya wananchi, basi maandamano mengine yatafanywa nchini humo tarehe 31 mwezi huu wa Januari, 2023.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *