Waandamanaji wa Italia walikusanyika katika mji wa bandari wa Genoa kuzuia upakiaji wa silaha zitakazotumwa kwa serikali ya Yemen iliyojiuzulu.
Raia wa mji wa Genoa nchini Italia walifanya maandamano siku ya Ijumaa asubuhi kupinga utumaji wa silaha kwa serikali ya Yemen iliyojiuzulu.
Wananchi wa Genoa, wakiwemo wanafunzi na wanachama wa vyama vya wafanyakazi, waliandamana hadi bandarini, wakiwa wameshikilia mabango yakiashiria ujumbe wa kupinga vita.
Waandamanaji hao walikusanyika mbele ya meli hiyo ya wafanyabiashara kupinga upakiaji wa silaha zitakazotumwa kwa serikali ya Yemen iliyojiuzulu.
Rasha Today aliandika; “Hatimaye, kutokana na shinikizo la waandamanaji na kuvurugika kwa shughuli za upakiaji, mchakato wa kupeleka silaha Yemen uliahirishwa,”.
Licha ya madai ya Saudia kusimamisha operesheni za kijeshi nchini Yemen, chanzo cha jeshi la Yemen kimesema kuwa, idadi ya mashambulizi mapya ya vikosi vya muungano wa Saudia kwenye maeneo ya kusini mwa Hudaydah katika siku iliyopita yamefikia 103.