Maelfu ya watu kutoka Johannesburg nchini Afrika Kusini walipiga nara dhidi ya jinai za utawala wa Kizayuni wa Ghaza kwa kufanya maandamano makubwa siku ya Jumamosi.
Maelfu ya wakaazi wa mji wa Johannesburg nchini Afrika Kusini walikusanyika mbele ya ubalozi mdogo wa Marekani katika mji huo Jumamosi na kutoa nara dhidi ya utawala wa Kizayuni.
Waandamanaji wamesisitiza kuwa, Marekani imekuwa ikitoa maelfu ya tani za silaha kwa utawala wa Kizayuni tangu mwanzoni mwa vita na kuichukulia Marekani kuwa mshirika wa utawala huo wa Kizayuni katika mashambulizi ya mabomu katika Ukanda wa Gaza.
Roshan Dado, mmoja wa viongozi wa vuguvugu la kuususia utawala wa Kizayuni amesema miongoni mwa waandamanaji hao: “Mpaka itakapohakikishwa kuwa usitishaji vita unapatikana katika Ukanda wa Gaza na misaada ya kutosha ya kibinadamu ifikie huko, maandamano yetu yataendelea hapa.”
Mnamo tarehe 29 Disemba, Afrika Kusini iliishutumu Tel Aviv kwa kuwauwa kwa umati Wapalestina katika Ukanda wa Gaza na kuishtaki Tel Aviv katika Mahakama ya The Hague. Kufuatia malalamiko hayo, mawakili wa utetezi wa Israel walifika katika mahakama hii jana kutetea utawala huu.
Hapo jana, baada ya utetezi wa mwisho wa Israel katika Mahakama ya Kimataifa ya Uadilifu, Waziri wa Sheria wa Afrika Kusini alisema kuwa, utawala wa Israel umepata kushindwa kwa njia ya kufedhehesha.
Hapo jana mwakilishi huyo wa Afrika Kusini alisisitiza katika kikao cha kwanza cha tuhuma za Israel katika Mahakama ya Kimataifa ya Uadilifu kwamba utawala wa Kizayuni unatekeleza siasa za ubaguzi wa rangi dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Ghaza.
Mwakilishi huyo wa Afrika Kusini alisema: “Tangu mwaka 1948, Israel imewahamisha na kuwatawanya watu wa Palestina kwa utaratibu na kwa makusudi kuwanyima haki yao ya kimataifa ya kujitawala… Tuna wasiwasi hasa kuhusu sheria na sera za kibaguzi za Israel.” ubaguzi wa rangi kwa watu wa Palestina.”