Maandamano ya maelfu ya Wazayuni yanaendelea katika ardhi za Palestina

Maelfu ya Wazayuni wameendelea na maandamano yao ya kumpinga waziri mkuu wa utawala wa Kizayuni, Benjamin Netanyahu, katika miji ya Quds na Tel Aviv licha ya kuweko sherehe za miaka 75 ya kuasisiwa utawala haramu na pandikizi wa Israel.

Tangu miezi minne nyuma, Wazayuni wanafanya maandamano kila wiki kupinga marekebisho ya serikali ya Benjamin Netanyahu katika mfumo wa mahakama wa Israel wakisema kukwa, marekebisho hayo yanakwenda kinyume na demokrasia.

Mapema leo Jumatano, televisheni ya Rusia al Yaum imeripoti kuendelea maandamano ya Wazayuni hao chini ya kaulimbiu ya “kuokolewa demokrasia.”

Kwa mujibu wa taarifa hiyo,  maandamano makubwa kama hayo yamefanyika kwenye miji mingine ya ardhi za Palestina zilizopachikwa jina bandia la Israel. Waungaji mkono wa marekebisho hayo nao wamepanga kukusanyika mbele ya majengo ya bunge la utawala wa Kizayuni, Knesset.

Tarehe 27 mwezi uliopita wa Machi, Benjamin Netanyahu alisitisha kampeni yake ya kuufanyia marekebisho mfumo wa mahakama wa utawala wa Kizayuni kwa tamaa ya kukomesha maandamano ya wapinzani, lakini maandamano hayo yanaendelea kwa nguvu kubwa zaidi.

Wapinzani wa Netanyahu wanasema kuwa lengo la marekebisho hayo ni kuvidhoofisha vyombo vya sheria na mahakama vya Israel na kumpa mwanya Netanyahu wa kukimbia kitanzi cha hukumu ya ufisadi inayomkabili.

Hivi sasa Netanyahu na familia yake wana kesi tatu za kujibu kuhusu ufisadi wa fedha na kula rushwa. Hatua ya Benjamin Netanyahu ya kujaribu kuudhoofisha mfumo wa mahakama wa utawala wa Kizayuni inatishia kuzuka vita vya ndani na kusambaratika utawala wa Kizayuni wa Israel.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *