Kwa mujibu wa ripoti hii, mwaka huu, baada ya mapumziko ya miaka miwili ya kufanya maandamano ya hadhara ya Siku ya Quds Duniani kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Corona, uratibu wa kimsingi ulifanyika ili kuandaa maandamano makubwa yatakayofanyika kwa wakati mmoja sawia na maandamano ya mji wa Tehran, katika zaidi ya miji 900.
Maandamano hayo pia yalifanyika katika zaidi ya nchi 90 yakihudhuriwa na Waislamu na watu wenye fikra huru kutoka kwenye dini nyingine kwa njia ya mikusanyiko na kulaani utawala wa Kizayuni wa mauaji ya watoto na kuwatetea wananchi madhulumu wa Palestina na Quds Tukufu.
Maandamano hayo ya Siku ya Quds yalifanyika katika Ubalozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Amman kwa kuhudhuriwa na shakhsia kadhaa wa kisiasa wa Palestina na Jordan.
Ripoti zimeeleza utayari wa Wapalestina kuadhimisha Siku ya Al-Quds katika Msikiti wa Al-Aqsa huku hatua kali za usalama zikiandaliwa na Wazayuni.