Madai ya London: Urusi inalenga kupenya ndani kabisa ya jimbo la Donetsk

Wizara ya Ulinzi ya Uingereza ilidai kuwa jeshi la Ukraine lilikuwa likipinga hatua ya Urusi kusonga mbele,  na kusema kua Moscow ilikuwa ikijaribu kuiteka Sverodontsk.

Wakati huo huo Waziri wa Ulinzi wa Urusi akitangaza kwamba vikosi vyake vinasonga mbele mashariki mwa Ukraine na kuchukua udhibiti wa maeneo 15 muhimu, London ilidai kwamba Warusi walikuwa wakijaribu kupenya ndani kabisa ya jimbo la Donetsk.

Pentagon ilisema katika taarifa yake kwamba mapigano katika eneo la Sverodontesk yaliendelea siku ya Alhamisi, lakini kwamba katika muda wa saa 48 zilizopita, kundi la wanajeshi wa mashariki mwa Urusi huenda wakaongeza juhudi zao za kusonga mbele kusini mwa Izium.

Kwa mujibu wa tovuti ya shirika hilo, taarifa hiyo ilidai kuwa kusonga mbele kwa Urusi kwenye mhimili wa Izium kumesitishwa tangu Aprili kwa sababu majeshi ya Ukraine yalitumia vyema uwanja huo kupunguza kasi ya Urusi.

Shirika la kijasusi la kijeshi pia lilitathmini kuwa Urusi ina uwezekano wa kutaka kurejesha kasi katika eneo hilo ili kuweka shinikizo zaidi kwa Sverodontesk na kuiruhusu kusonga mbele zaidi katika eneo la Donetsk.

Wizara ya Ulinzi ya Russia pia ilitoa takwimu mpya kuhusu vita vya Ukraine, ikisema kuwa vikosi vya Ukraine vimepata hasara kubwa katika masuala ya vifaa vya kijeshi na wafanyakazi katika eneo la mashariki mwa nchi hiyo.

Mnamo Februari 24, Ofisi ya Rais wa Urusi iliamuru kuanza kwa operesheni za kijeshi nchini Ukraine, ikiomba msaada wa jamhuri za Donbass za Luhansk na Donetsk kwa ajili ya ulinzi dhidi ya Ukraine, na alisisitiza tangu awali kwamba Moscow haitaki kuteka eneo la Ukrain, na kusema kwamba madhumuni ya operesheni hiyo ya kijeshi ilikuwa kuizuia Ukrain kumiliki silaha.

 

 

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *