Madhumuni ya kusimamisha uadilifu katika jamii kwa mwanasosholojia na Qur’an: Hujjatul Islam Ustad Syed Jawad Naqvi

Hujjatul Islam Ustad Syed Jawad Naqvi
(Principal Jamia Orwatul Wuthqa – Lahore)
Delivered at: Masjid Baitul ul Ateeq
Lahore – Pakistan

Hotuba ya ijumaa – 2nd February, 2024

Hotuba ya 1 : Madhumuni ya kusimamisha uadilifu katika jamii kwa mwanasosholojia na Qur’an
Hotuba ya 2: Kushiriki katika uchaguzi ni unyakuzi wa haki za uimamu
Taqwa ( uchamungu ) sio kujizuia, uoga bali ni ulinzi hata hivyo uoga na kujizuia ni mambo muhimu sana ya usalama. Maisha ya akhera ambayo ni matokeo ya maisha haya ya dunia yanapata ulinzi wake kutoka kwenye Taqwa. Uadilifu ndio msingi wa kuwa na uchamungu na kuudumisha.na Qur’an inasema kuwa uadilifu upo karibu sana na uchamungu (Taqwa) uadilifu ndani ya ulimwengu mbali na maisha ya binadamu Mwenyezi Mungu ndiye mwenye kusimamisha uadilifu hali ya kuwa kwa mwanadamu uadilifu unatendeka kwa matakwa na nia. Sio jambo la mtu mmoja mmoja bali ni lengo la kijamii ambayo inabidi isimamishe uadilifu kisha uchamungu.
Mpango ambao ameupanga Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kusimamisha uadilifu umeelezewa katika Aya ya 25 ya surat Al-Hadid
لَقَدْ أَرْسَلْنَا رُسُلَنَا بِالْبَيِّنَاتِ وَأَنْزَلْنَا مَعَهُمُ الْكِتَابَ وَالْمِيزَانَ لِيَقُومَ النَّاسُ بِالْقِسْطِ ۖ وَأَنْزَلْنَا الْحَدِيدَ فِيهِ بَأْسٌ شَدِيدٌ وَمَنَافِعُ لِلنَّاسِ وَلِيَعْلَمَ اللَّهُ مَنْ يَنْصُرُهُ وَرُسُلَهُ بِالْغَيْبِ ۚ إِنَّ اللَّهَ قَوِيٌّ عَزِيزٌ {25}
Kwa hakika tuliwatuma Mitume wetu kwa dalili waziwazi, na tukateremsha Kitabu pamoja nao na Mizani, ili watu wasimamie uadilifu, na tumeteremsha chuma chenye nguvu nyingi na manufaa kwa watu, na ili Mwenyezi Mungu amjue anaye mnusuru Yeye na Mitume wake kwa ghaibu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu Mwenye kushinda.
Mwenyezi Mungu anasema tumewatuma Mitume wetu kwa hoja zilizo wazi za kusimamisha Uadilifu, na tumewapa Kitabu na kisha Mizani ambayo ni dini ili watu wainuke juu na kwa uadilifu, hivyo basi waweze kuanzisha jamii kwa misingi ya uadilifu. Jambo la nne ambalo tumewapa Mitume ni Chuma ambacho ni upanga ambacho kinamaanisha nguvu, shinikizo na dhiki vyovyote iwavyo mnatakiwa kusimamisha uadilifu katika njia hii. Kwa mujibu wa Quran haki ya kimsingi ya mwanadamu ambayo mtu anatakiwa kuidai ni uadilifu. Kuna dini, Quran, Mitume, Maimamu na kisha upanga, nguvu zote ni kwa ajili ya kusimamisha uadilifu.
Nafasi ambayo Mwenyezi Mungu ameiweka ambayo lengo lake pekee ni kusimamisha Adl. Mtume ana makusudio ya kupokea dini kutoka kwa Mwenyezi Mungu, kuieneza na kisha kuisimamisha. Maimamu wanapaswa kutekeleza, kusimamisha uadilifu na kisha kuongoza kwa misingi ya uadilifu. Kwa mujibu wa kanuni hii ya Qur’ani tunaweza kuona tofauti za serikali zenye msingi wa uadilifu. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alianzisha jumuiya ya kwanza ya waumini. Aliigeuza jamii ya Jahiliyya kuwa jamii ya uadilifu. Lakini baada ya Mtume (s.a.w.w.) watu waliishikana mikono na kuanza kuwachagua maimamu wao wenyewe. Kwa Shia ukhalifa unatoka kwa Mwenyezi Mungu na Ali ameainishwa na Mwenyezi Mungu katika kwa Ushahidi lukuki ikiwemo tukio la Ghadir. Lakini ulianzishwa mfumo tofauti ambao unaitwa khilafa.

Unapotazama kipindi cha Mtume( s.a.w) jamii ya makhalifa na jamii ya Ali (a). Pindi IMAM Ali alipochukua madaraka baada ya miaka 25 alisema: hali yenu leo hii ni kama ya kipindi cha kabla ya kuja Mtume (s.a.w) Qur’an ilishalitabiri hili pia kunako mnacho takiwa kufanya baada ya Mtume. Mambo yote ya muonekano wa nje kama ibada n.k. yaliendelea katika kipindi cha makhalifa na hata mambo mengine kama kushinda na kuziteka nchi nyingine na kupanua nchi za Kiislamu kuliongezeka. Sasa kwanini Ali anasema kwamba hali yenu ni kama hali ya zama za jāhiliyyah. Anaichambua jamii kwa kutumia msingi wa uadilifu ambao ulikuwa umetelekezwa. Hivyo aliibuka na msingi wa uadilifu na kujaribu kusimamisha uadilifu. Lakini wale ambao hawakuwa tayari kukubali uadilifu walimpiga vita. Kumbuka kwamba vita vyote vya Imamu Ali vilikuwa ni vita vya ndani. Makundi matatu ya Mariqina, Nakithina na Qasitin wote walikuwa na upinzani wa namna moja kwa Ali ambao ulikuwa umetokana na mazoea ya tabia ya kutokuwa na uadilifu, Ali (a.s) alitaka kutatua hayo yote kwa msingi wa uadilifu. Hiki ndicho kitu ambacho walikuwa hawakikubali. Wanasiasa wakongwe wa zama hizi walimshauri Imam Ali kuachana na suala la uadilifu na kujaribu kujikita katika kuimarisha mamlaka. Mtazamo wa Maimamu Ali (a.s) ulikuwa tofauti. Alisema: ikiwa siwezi kusiamisha uadilifu kupitia uongozi , basi uongozi huo thamani yake inashindwa hata kiatu changu hiki kilicho chanika.
Kwa Ali (a.s) hakuna kitu kinachoweza kuathiriwa kwa sababu ya madaraka. Usitoe mali, maisha au maadili kwa ajili ya kupata madaraka. Leo hii tupo tayari kutoa kila kitu muhanga kwa ajili ya madaraka. Nakithina ni wale waliovunja kiapo chao cha utii kwa Ali (a.s) hawakuwa maadui bali walikuwa ni wenye kumuunga mkono na kumuingiza madarakani, lakini walivunja kiapo chao cha utii, wakatengeneza jeshi kwa ajili ya kupambana dhidi ya Ali. Hali hiyo inaweza kuonekana kwa maimamu kwamba wale waliotoa kiapo ncha utii walikuja kukabilana na Ali. Na katika mapinduzi ya Kiislamu pia tunaweza kuona kwamba waliokuwa walikwenda kinyume baada ya mapinduizi kwa kuvitaka vitu vya kimaada wakasimama dhidi ya mapinduzi. Hivyo kundi la Makhawariji lilikuwa ni kundi la wajinga, na pindi waislamu wanapokuwa wajinga wanakuwa ni hatari zaidi ya adui mwingine yeyote. Jeshi hili la watu 12000 halikutoka SYRIRA bali lilitokana na ujinga kupitia propaganda za adui. Hivi imam aliposimama ilikuwa ni kwa ajili ya uadilifu.
Imamu wa zama ana agenda moja ambayo ni kusimamisha uadilifu. Jamii zinapambanuliwa na kujulikana kwa uadilifu. Wanasayansi ya jamii wanaamini ya kwamba jamii inaweza kustawi na kukua kwa msingi wa uadilifu. Kama unataka kutathmini jamii zetu kwa kanuni za kijamii, kitu cha kwanza kuonekana inatakiwa kiwe ni uadilifu kama kitu hicho kipo ndani ya misingi yake, katika idara na vitengo mbalimbali. Wanasosholojia wana mitazamo miwili katika vya kuwepo kwa uadilifu ndani ya jamii. Hawazingatii uadilifu kama ni lengo bali ni kama nyenzo. Katika dini pia uadilifu sio lengo la mwisho bali ni nyenzo ambayo kupitia kwayo unatakiwa kufikia lengo. Lengo la mwisho lina malengo mengi tangulizi ambapo unalifikia lengo la mwisho kwa hatua. Ni kama unavyo safiri unapitia vituo vingi hadi ufike kituo cha mwisho.
Hatua za kati za nyenzo lakini pia ni malengo. Kama wanaoenda Karbala huenda Kufah kwanza lakini hili sio lengo halisi la mwisho. Ni nyenzo amabayo kupitia kwayo unatakiwa kufikia kituo kifuatacho. Lengo moja ndilo halisi na la mwisho ni ambapo safari inaishia lakini vituo fulani ni malengo ya kati. ‘Allama Iqbal amelitaja jambo hili zuri kwamba jamii inatakiwa ianzishe utaratibu wa kudumu na malengo, yaani lengo baada ya lengo. Ikiwa jamii itafikia lengo halafu ikasimama hapo basi hicho ndicho kifo cha jamii. Ikiwa utafikia lengo la mwisho hutakiwi kusema sasa nimeshafika na kwa sasa uanatakiwa kulala. Kuna lengo baada ya lengo hadi kufikia lengo la mwisho.
wanasayansi wa kijamii wanaomchukulia mwanadamu kama mpenda mali na aliumbwa kwa bahati mbaya na mwendo wa maada. Kwa wao wana mitazamo miwili mmoja ni wa kibepari na mwingine ni wa ujamaa. Wanasayansi wote hawa wawili wanauzingatia uadilifu kuwa ni msingi wa jamii lakini lengo ni kitu kingine. Je ni nini lengo la uadilifu ndani ya Qur’an? Je uadilifu ni lengo au ni nyenzo ya kufikia mahala fulani? Kwa dini uadilifu ndilo lengo la msingi ambalo kupitia lengo hilo tunatakiwa kufikia lengo la mwisho.

Ubepari unazingatia uadilifu kuwa ni jambo la lazima katika jamii ili mtu aweze kupata uhuru kutoka kwenye sheria na vizuizi. Maisha ambayo mwanadamu atakuwa yupo huru kutokana na sheria, dini, maadili na mengineyo yaani mtu aweze kufanya chochote anachotamani kukifanya. Ndani ya dini kuna utakatifu mbalimbali lakini katika uliberali jambo takatifu kwao ni ukombozi. Hapa ukombozi haumaanishi uhuru bali unamaanisha kutofungwa na sheria yeyote. Hakutakiwi kuwa na kizuizi chochote mbele ya matamanio yake. inabidi kutengeneza jamii ambayo mtu atakuwa huru kufanya chochote anachotaka. Kwa mfano Hutakiwi kumzuia mwanaume kuolewa na mwanaume mwenzake au kuoana na mnyama. Hivyo basi matamanio ya mtu ndio lengo halisi na wanahitaji uadilifu kwa ajili ya uhuru wa hali hii. Kwao ikiwa mtu anataka kujilimbikizia utajiri ni sawa anaweza kufanya na kama anataka kupoteza utajiri pia anaweza kufanya hivyo, anataka kuwatawala wengine kwa mabavu anaweza kufanya na huwezi kumzuia kufanya haya.
Kwa ujamaa wanasayansi wanasema lengo halisi na la mwisho ni kutimiza mahitaji muhimu ya mwanadamu. Hakuna maisha ya kiroho na hakuna maisha baada ya maisha ya kufa. Vyakula na madawa ni mahitaji muhimu ya mwanadamu. Uadilifu hapa unamaanisha inabidi mtu awe na mahitaji yake muhimu. Katika ubepari mtu anaweza kufanya chochote anachotaka. Na matamanio yake hayazuiliwi na mahitaji, wamekupeleka mbali zaidi ya mahitaji bali wanasema mahitaji yanasimama yenyewe . sheria na dini husimamia mahitaji ya mwanadamu. ni yapi mahitaji ya mtu mgonjwa? Daktari ndiye anayesema. Katika ubepari msingi wa mahitaji ya mtu ni matamanio yake, lakini katika ujamaa jamii ndio inaamua kunako mahitaji ya mtu na mtaji wote utatawanywa kwa baina ya wahitaji na kitakacho salia kitabaki serikalini.
Qur’an inasema tumewatuma mitume, kitabu na chuma ili muweze kusimamisha uadilifu. Kwanini mnahitaji uadilifu? Kwa dini uadilifu ni nguzo ambayo kwayo mtu anaweza kufikia lengo kuu la kuumbwa. Ndani ya dini mahitaji ya kila mtu inabidi yatekelezwe, kama Qur’an inavyosema kuhusu ndugu, haki za mayatima, majirani na masikini wanatakiwa kutazamwa kwa ukaribu na kuwajali. Lakini mahitaji sio lengo la uadilifu bali hutumika ili kuweza kufikia lengo halisi la kuumbwa mwanadamu. moja ya malengo makuu ni kukutana na Allah ( Liqaullah). Baadhi ya watu wanafikiri liqau kuwa ina maana ya kukutana na fadhila na thawabu za Mwenyezi Mungu. Neno Liqaullah limetumika katika Aya nyingi sana ndani ya Qur’an. Na lengo jingine kuu na la mwisho la mwanadamu ni ukamilifu ambao ni ukamilifu wa mwanadamu. Mwenyezi amembuni na kumpa umbo mwanadamu, akatengeneza mbegu ya ubinadamu na kumwambia mwanadamu kuwa mwanadamu mwenyewe. Pindi mtoto anapozaliwa ni mbegu ambayo imezaliwa ambaye tunamchanganyia vitu kadhaa ambavyo tunatengeza uji kutokana na vitu hivyo. Mtu atakuwa binadamu pale tu ambapo mbegu itapandwa kwenye udongo sahihi. Na udongo huo ni uadilifu. Ikiwa mbegu hii itapandwa kwenye shamba la uadilifu, mbegu hiyo itafikia ubinadamu na liqau. Mwenyezi Mungu anakutana na kila binadamu lakini sio mbegu. Lengo kuu la kuumbwa mwanadamu aliloliweka Mwenyezi Mungu ni liqau, ukamilifu, ukuruba na haya yote hutokea kupitia uadilifu.
Imamu ni mlezi wa jamii ambaye bila shaka kapewa mamlaka na Mwenyezi Mungu. Unasoma Qur’an, dini na kuvaa kilemba kisha unachukua mamlaka kutoka kwa imamu na kumkabidhi Taghuti ( shetani) utapiga kura sasa, kwa hiyo hii ina maana gani? Maana yake unachukua mamlaka kutoka kwa aliyepewa mamlaka na Mwenyezi Mungu. Ambaye mwenyezi Mungu kamfanya kuwa kiongozi, sasa kwanini usiisalimishe jamii kwake ? ni kwa sababu atakuja kusimamisha uadilifu, na pindi uadilifu utakapokuwa juu, tutapinga kwa sababu maslahi yetu hayapo kwenye uadilifu bali yapo kwenye kutotenda uadilifu na dhuluma. Sababu ya maulama kwenda kwenye hukumu za kinchi, ufalme ni kwa sababu ya maslahi yao binafsi na sio kwa ajili ya dini. Tunaweza kuona namna gani watu wengi walimuacha imamu Ali na kwenda kwa Muawiya kwa sababu ya maslahi yao binafsi. Alikuwa akiwakirimu kwa vyakula vizuri na Muawiya alikuwa anapenda sana kusikia maneno mabaya kuhusu Ali. Yeyote ambaye angemponda Ali basi angefurahikiwa na kupewa zawadi. Kuna Muawiya wengi katika historia na watu wenye kuendea maslahi binafsi. Kuwa mbali na maimamu kuna sababu moja tu nayo ni maslahi binafsi.
Ali anasema yeyote anaye fikiri ya kuwa uadilifu ni mgumu basi dhuluma itakuwa ngumu zaidi. Hili lilitokea. Mwaka 2018 nilisema muwe mnaweka kumbukumbu za tarehe na viwango vya vitu na kisha katika uchaguzi ujao mfanye mahesabu tulikuwa wapi na leo tupo wapi. Na sasahivi mwaka huu Februari 2024 chukua kumbukumbu ya wapi tulipo na kisha baada ya miaka mitano fanya mahesabu. Ni Taghuti baada ya Taghuti na mmemsubirisha Imamu. Imamu yupo tayari kwa ajili ya kusimamisha uadilifu lakini sisi hatuko tayari. Pindi uchaguzi unapofanyika moyo wa Imamu huumia. Pindi Musa awaonapo watu wamemzunguka Saamiriy moyo wake huvunjika. Hivyo basi msitaraji kwamba imamu atatufurahia na atarudi kwetu. Mwenyezi Mungu atupe ufahamu wa Qur’an na dini na kuifahamu dini kwa kupitia mafunzo ya Ahlul-Bayt(a).

Hotuba ya 2
Allah ameweka usalama wa jamii ya mwanadamu katika mikono ya mwanadamu mwenyewe kupitia uchamungu. Hii ni kwa sababu mtu amepewa hisia, nia na mapenzi au utashi. Lakini mwanadamu ameuweka mfumo wa kimungu nyuma na badala yake akaweka mfumo wake mwenyewe hivyo imekuwa fedheha. Leo tunaweza kuona kuna wanyama, wenye majina ya kishenzi ambao mfano wao mkubwa ni Ghaza na nchi nyinginezo kama Iraq, Lebanon, Kashmir na Yemen. Uchokozi mkubwa zaidi upo Ghaza na binadamu wote wanathibitisha ubinadamu wao ambao umekufa. Kuna watoto na akina mama ambao wanauliwa kila siku na hawa wanyama, mashetani wanafanya na wengine wamekaa kimya wakitoa ushahidi juu ya jinai zao. Wanataka kufuta kabila na kizazi hiki ulimwenguni. Ni idadi kubwa sana ya watu wanaokufa tukihesabu na wale ambao wanakuwa ni majeruhi, wagonjwa, upungufu wa chakula ambao wanaweza kuwa zaidi ya 100,000. Na kila mtu anahusika na jinai hii. Wale wanaotenda dhuluma , wanao wasaidia na kuwaunga mkono na wanaokaa kimya. Kwa upande wa Shia tunasema laana ziwaendee wauwaji, madhalimu na wale wanaobaki kimya baada ya kusikia dhuluma hii. Ukimya wao ni ishara ya kukubaliana. Wanafanya ushenzi huu kwa sababu ya hii fedheha.
Ukiacha mfumo wa Mwenyezi Mungu basi tija yake haya ndio yanayo tokea. Demokrasia ipo Israel.Uk, USA na uharibifu wote huu unafanywa na viongozi ambao wamechaguliwa kwa demokrasia. Ni nani atasimamisha jinai hii? Imamu anayesema kuwa ikiwa kikuku cha mguu wa mwanamke wa Kizayuni kitaibiwa basi muumini anatakiwa afe kwa aibu. Wanademokrasia wote wapo kimya ni watazamaji tu. Tunaweza kuona tarehe 8 Februari nini kitatokea. Kuna wagombea ambao hawana thamani ya kutaja majina yao. Unaweza kuona kwenye media ni upuuzi wanao uogea wagombea hawa ni uhalisia wa upumbavu. \Allama Iqbal anasema
Guriz az Tarz e Jamhoori, Gulame Pukhtekaari sho
Jitoe kwenye demokrasia , ikimbie. Huyu ni Iqbal ambaye ni mbunifu wa Pakistan. Ndiye mtu ambaye alipandikiza mbegu kwenye vichwa vya Wahindi kutengeneza nchi yao wenyewe. Na pindi mtakapo fanikiwa kisha ilindeni kutokana na demokrasia na badala yake kuweni wafuasi wa mtu aliye pevuka. Ambaye ana mafungamano na Mwenyezi Mungu ndiye aliye pevuka ambao ni uimamu.
Kisha baadaye anasema
Az do sad Khar Kaare Insaani Nami aayad
Punda mia mbili hawawezi kufanya kazi au kufikiri hata kama mtu mmoja
Sikiliza tu upuuzi wa hawa wanasiasa, hata Allama angeweza kubadili neno punda kwa kitu kingine. Kuna wengine ambao wanaongea kama mapunda, je unataraji kutoka kwa mapunda hawa wataweza kuikomboa Pakistan na kukuza uchumi. Hawa viwete wanakaa na kwenye TV masaa na kuzungumzia matatizo ya Pakistan na kusema kwamba waliosababisha ni wale walioko jela. Hivyo suluhisho ni kuwa na uchaguzi safi, kisha watakuja wale watu wabaya madarakani kutatua matatizo?

Pointi ya pili niliyo itaja ilikuwa kama ni haki ya nani unampa. Mwenyezi Mungu amewapa haki jamii ya wanajamii kwa wali. Mashia, Masunni , waandishi wa itikadi na wa fiqh wanapoelezea kuhusu uimamu wote wanakubaliana kwamba uimamu ni utawala, utawala wa ulimwengu na dini. Mmekabidhi taifa, watu na uchumi kwenye mikono ya Taghuti? Wanachukua majina ya maimamu kama Imamu Husayn kwa ajili ya kutafuta kura kwa ajili ya Taghuti. Nyinyi ni sehemu ya jinai. Unapotoa haki ya Imamu kumpa mtu fulani hivyo basi wewe mwishowe utakwa wewe ndio muhalifu. Haki za Imam ni kwamba unatakiwa kufanya kila kitu uwezacho ili kusimamisha uadilifu.
Ulimwengu mzima una wajibu mmoja ambao ni kwa ajili ya Palestina. Kama mfano: ikiwa msikiti utanajisika kama kapeti au baadhi ya sehemu yake: na unakuja kusali ukiwa unajua kwamba msikiti umenajisika. Mafaqihi wengi wanasema kwamba sala hii haitasihi kwa sababu wajibu wa kwanza ilikuwa ni kuusafisha msikiti. Baadhi ya mafaqihi wanasema sala inaweza kukubalika lakini kuna uasi na madhambi kwa kuwa umeacha kufanya jambo la wajibu. Inatakiwa tuzifahamu sheria hizi. Leo hii maulama wote wameshughulishwa na uchaguzi. Majukumu yenu ya kwanza na ya kipaumbele ni kusimama kwa ajili ya Palestina. Wanawake wengi na watoto wanauliwa na wanakufa kila siku, hivyo ni wajibu wetu kuwatelekeza na kujishughulisha na uchaguzi.
Tarehe 8 Februari waumini wanatakiwa kusimama kwa ajili ya Palestina. Kwanza fanya hili kwa ajili ya kuwaokoa na kisha ndio ufanye mambo mengine. Mmeacha hili na kuwa sababu ya taifa kukosa baraka. Ni nani walifanya usaliti kwa Palestina na Kashmir? Ni mataghuti hawa hawa ambao mnawafuata. Jahazi la uokovu ni Ahlulbayt na hili hutokea unapokuwa chini ya mfumo wa uimamu wa Ahlulbayt na sio tu kuishia kuwaomboleza tu.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *