Maelfu ya visa vya unyanyasaji wa kingono dhidi ya wagonjwa yaripotiwa nchini Uingereza

Data mpya zinaonyesha kuwa tangu 2017, kesi 16,082 za unyanyasaji wa kingono dhidi ya madaktari, wauguzi, wagonjwa na wahudumu wa afya zimeripotiwa katika hospitali za Uingereza.

Kulingana na gazeti la Telegraph, kila wiki kunaripotiwa visa sita vya unyanyasaji wa kingono wa wafanyakazi wa Huduma ya Taifa ya Afya (NHS) dhidi ya mgonjwa nchini Uingereza.

Takwimu mpya zinaonesha kuwa takriban theluthi moja ya taasisi za afya za Uingereza zimerekodi ongezeko la unyanyasaji wa kijinsia tangu 2017, wakati mamilioni ya dola yametumiwa na Huduma ya Taifa ya Afya (NHS) katika kipindi hicho kushughulikia malalamiko ya kisheria kuhusu unyanyasaji wa kingono.

Waziri wa Afya wa Uingereza, Steve Barclay, amesema matokeo hayo yanatia wasiwasi na ametoa wito kwa viongozi wa NHS “kuchukua hatua kali” za kukabiliana na matukio kama hayo ndani ya shirika hilo.

Jumuiya ya hisani ya kutoa elimu ya usalama wa wagonjwa imetangaza kuwa: Ufichuzi huo unaotia wasiwasi sana wa Telegraph umeonyesha matumizi mabaya ya “kutokuwapo mlingano wa nguvu” kati ya wagonjwa walio katika mazingira magumu na watoa huduma za afya.

Kashfa za kimaadili na ufuska zimekithiri sana nchini Uingereza hadi kwenye familia ya kifalme ya nchi hiyo.

Mapema mwezi Aprili mwaka huu Netflix, jukwaa la uzalishaji na usambazaji wa filamu na dokumentari la Marekani, iliweka wazi uhusiano kati ya genge la kunyanyasa watoto na familia ya kifalme ya Uingereza katika filamu ya dokumentari iliyoibua utata na mjadala mkubwa.

Filamu hiyo ya Netflix ilifichua barua za hati za mkono baina ya Mfalme Charles, mtoto mkubwa wa kiume wa aliyekuwa wa malikia wa Uingereza, Elizabeth II, na kinara mkubwa wa ufuska na ufisadi katika vyombo vya habari, Jimmy Sevile, katika miaka ya baina ya 1986 na 2006.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *