Mafanikio ya kihistoria ya Iran na watu wanapaswa kuandaa ziara ya Rais Raisi kuja Pakistan: Ustad Syed Jawad Naqvi

Hujjatul Islam Ustad Syed Jawad Naqvi

(Principal Jamia Orwatul Wuthqa – Lahore)
Imetolewa : Masjid Baitul ul Ateeq
Lahore – Pakistan

Hotuba ya Ijumaa – 19 April, 202

 

Hotuba ya 1: Maana ya Tawakkul katika Qur’an
Hotuba ya 2: Mafanikio ya kihistoria ya Iran na watu wanapaswa kuandaa ziara ya Rais Raisi kuja Pakistan.

Sehemu moja ya Taqwa ni uwanja wa ulinzi ambapo muumini anatakiwa kukabiliana na maadui. Njia ya Imani ina uhitaji huu muhimu kwamba katika kila hatua atapaswa kukabiliana na maadui. Imani haifanyi yeyote kuwa adui lakini makafiri hawawezi kuwavumilia waumini na hapa ndipo unapoibuka uadui. Qur’an inasema kwamba wafalme, watawala, na wasomi siku zote ndio waliokuwa na uadui kwa mitume. Uadui mkubwa ambao Qur’an imeutaja ni wa Shetani ambao ni alama ya uwasilishaji na katika uhalisia ni uadui wa mwanadamu kumuelekea mwanadamu. Mbali na mwanadamu kuna majini ambao hawatambuliki na hawaonekani. Malaika sio maadui wa mwanadamu. Kisha kuna maluweluwe mengine kama wachawi, misukule na vitu kama hivyo ambavyo havina uwepo wowote . uadui wa mwanadamu kwa mwanadamu ni unatokana na Imani. Ikiwa mtu sio muumini basi uadui utaishia hapo. Katika uwanja huu waumini huwatawala maadui na wakate mwingine maadui huwaangusha waumini. Leo hii tunaona kwa mujibu wa kigezo vya Qur’an idadi ya waumini ni ndogo lakini ikiwa tutamzingatia kila anayeitwa Muislamu kuwa muumini kwa ujumla basi wote ni wenye kutawaliwa na wengine. Wale ambao ni waumini wa kweli kwa mujibu wa Qur’an ndio wenye kufanyiwa uadui zaidi. Na sio muhimu kwamba ukiwa katika njia ya haki utakuwa ni mwenye kutawala kwa sababu Qur’an imeelezea masharti na vigezo ambavyo ikiwa utakuwa navyo uatawala.
Ikiwa muumini atatawala basi kwa mujibu wa Surah Maida vigezo vitakuwa ni Tawakkul na Taqwa.

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اذْكُرُوا نِعْمَتَ اللَّهِ عَلَيْكُمْ إِذْ هَمَّ قَوْمٌ أَنْ يَبْسُطُوا إِلَيْكُمْ أَيْدِيَهُمْ فَكَفَّ أَيْدِيَهُمْ عَنْكُمْ ۖ وَاتَّقُوا اللَّهَ ۚ وَعَلَى اللَّهِ فَلْيَتَوَكَّلِ الْمُؤْمِنُونَ {11}
Enyi mlio amini! kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu iliyo juu yenu, walipo dhamiria watu kukunyosheeni mikono yao, na akaizuia mikono yao kwenu, na mcheni Mwenyezi Mungu. na Waumini wamtegemee Mwenyezi Mungu.

Enyi mlio amini! Pindi maadui wanapo kukunyosheeni mikono, Allah aliizuia mikono yao na hawakufanikiwa kukutokomezeni. Hivyo sasa kuwa na Taqwa na Tawakkul kwa Allah kwa sababu muumini anatakiwa kuchukuwa sera hizi mbili kwa ajili ya maisha ya kijamii. Hii Taqwa na Tawakkul inatakiwa zitokee katika Qur’an na sio kutoka katika Nyanja nyingine kama vile maadili na usufi. Elimu ya usufi ni tofauti na masufi ambao tunawaona ambao leo hii wametengeneza picha ya kujinyima ili kuwapotosha watu. Unyonge wa kiakili ni Wagnostiki ambao ni utambuzi wa uwepo wa Mwenyezi Mungu na kupata ukaribu wa mwanadamu na Mwenyezi Mungu. Kwa w2ale ambao wamesoma sayansi ya ascetism, wanatambua kuwa masufi ni wachache kwa wale ambao wamesoma mada hizi mbili Tawakkul na Taqwa zinajadiliwa kwa kina zaidi kama elimu ya ulinganisho wa sayansi ya kimaadili. Wasomi wa sayansi huzungumzia juu juu na sio kwa kina lakini wanafalsafa huzama ndani na kulizungumzia kwa kina zaidi katika kulidurusu jambo hili. Kama hauna utambuzi wa haya mambo mawili basi huwezi kutofautisha.
Tawakkul imejadiliwa na Masufi, maadili na Qur’an. Maana ya Tawakkul na Taqwa ambayo ipo katika akili zetu ni ile inayo tokana na maadili hivyo basi tunaopaswa kusoma mambo haya mawili kutoka katika Qur’an. Hii ni kwa sababu Qur’an haikuyachukua haya kutoka kwenye sayansi ya kiakili bali badala yake sayansi ya kiakili ndio imechukua kutoka kwenye Qur’an. Tunaona kama vitu hivi viwili vinakabiliana kwa sababu tafsiri ya Qur’an inatolewa kwa kutegemea Fiqh na maadili. Sayansi zimechukua mambo haya yote kutoka kwenye Qur’an na kisha kujitengenezea istilahi zao kitu ambacho ni haki ya kila sayansi kufanya hivyo.

Allah ameamrisha Taqwa na Tawakkul katika maisha yetu ya kila siku ambayo haijawekewa muda maalumu kama kusali bali ni katika mambo yetu yote ya kimaisha. Ibada ambazo zimewekewa muda maalumu ni kwa ajili ya kukupa mazoezi lakini thamani yake halisi huendelea na hujielezea kama msingi wa maisha ya mwanadamu. Sio kwamba inabidi upate Taqwa na Tawakkul mara tano au kumi kwa siku na hii ni kwa sababu ni sera na ni msingi wa maisha ya mwanadamu. Ufahamu wa jumla kuhusu Tawakkul ambao upo katika akili zetu ni huonekana kuwa ni kitu ambacho hakiwezekani kufanyika ambapo wengine pia hawasaidii, basi unatakiwa kumuamini Allah na kisha subiri mambo yafanywe na Allah. Hivyo kwetu sisi Tawakkul ina maana tu ya kumuamini Allah katika akili zetu. Ni kama tunavyofanya kwa watu kwamba tunawapa kazi na kusubiri kazi ifanyike kwa kumuamini . hii sio sera ya Tawakkul.

Katika istilahi Tawakkul inatokana na Tawkeel ambayo ina maana ya kukabidhi kitu au mambo kwa mtu fulani. Na sio uaminifu kwa sababu unapokabidhi kisha ndipo huja sifa muhimu ya kuamini katika kukabidhi. Unapo mkabidhi mtu kazi haina maana kwamba wewe unakata mahusiano na hiyo kazi kwamba sasa sio kazi yako ni kazi ya yule. Mamlaka ya kazi hiyo anakuwa kapewa mtu huyo kama tunavyo kabidhi mafaili kwa wakili ili azungumze kwa niaba yetu mahakamani na kututetea. Lakini bado hilo begi linakuwa ni miliki ya mteja. Kuwa na Tawakkul maana yake ni kwamba Allah ni wakili. Kwa namna tunavyofanya kwenye mahakama hiyo haina maana ya Tawakkul. Kinachotokea mahakamani ni mkataba ambao unauingia wewe na mwanasheria wako. Hiki ni kitu ambacho na wewe ungeweza kukifanya kama ungekuwa na elimu lakini umemweka mtu wa kulipwa ambaye anasimama badala yako. Na tunafanyiwa mambo kwa kulipa kama vile kuendesha gari na kuosha vyombo nyumbani na mengine tunayafanya wenyewe. Kufanywa kazi yako na mtu mwingine kwa kumlipa ni tofauti na wewe unavyofanya mwenyewe.
Tawakkul ina maana ya kumkabidhi mtu kazi yako na sio kwa msingi wa fidia. Tawakkul ni sifa ya mtu wa kawaida lakini wasomi wameenda juu zaidi katika mjadala huu. Pindi mtu wa kawaida anapo takiwa kuwa na Tawakkul basi inatakiwa ifahamike kwa mtu wa kawaida pia. Ebu tujaribu kufahamu Tawakkul kwa kutumia mfano. Tunaona meli zikielea baharini na kufanya safari zake na kila mtu ameshuhudia. Unaweza kuona kwamba Meli hizi ni nzito katika tani nyingi. Meli hii inafanya safari baharini na haizami , na Allah pia anasema kwamba kuelea kwa Meli hizi pia ni dalili ya uwepo wa Allah. Inatosha sana kufikiria kwamba kokoto na misumari huzama kwenye maji lakini meli hii nzito kiasi hiki haizami kwenye maji. Kuna kanuni ambayo iligunduliwa na mwanasayansi Mgiriki Archimedes. Kwa meli kuna mambo mawili kitu cha kwanza ni kwamba ina msongano na cha pili ina kipimo ( vipimo vitatu vya kila kitu n.k urefu , upana na kina). Kama kipimo cha kitu kinaweza kuwa kikubwa sana lakini msongano ukawa mdogo. Kama unavyoweza kuona kwamba muundo wake umetengenezwa kwa mbao, zina uzito mdogo hata ikiwa ni kubwa. Ikiwa matirio yana msongo kidogo ukilinganisha na kipimo chake na kukiweka kwenye maji hayo, basi kipimo chake hufunika maji. Kipimo cha meli au ukubwa wake hufunika sehemu ya maji. Pindi meli zinapo tengenezwa, kuta za meli hutengenezwa kwa tabaka mbili kukiwa na uwazi ndani yake. Sehemu ya chini ya meli huwa na nafasi ya wazi kwenye bodi. Bodi ya meli huonekana kuwa kubwa lakini ndani yake kuna msongano mdogo lakini bado ina uzito wa maelfu ya tani. Hakuna uzito wa kipimo lakini uzito ni wa melokuli ni mdogo kulinganisha na ukubwa wake. Pindi meli inapoingia majini sehemu yake ya chini hugusa maji na huzama ndani kidogo na maji kupita upande na kutokea upande mwingine. Kanuni ya Archimedes inasema kwamba uzito unaouweka juu ya maji ndio huo huo maji yake hupenya kwenye pembe zote na meli haitazama. Hii ni kwa sababu uzito huweka msukumo juu ya maji na kuna msukumo wa juu ya maji ambao huja kutoka kwenye maji kuelekea msingi wa meli na huzunguka katika pande za meli zote na ndio huifanya meli isizame kwenye maji.

Huu ni mfano ambao nimeutoa kwa ajili ya Tawakkul. Allah ameumba maji na kuyawekea kanuni. Kitu chochote ambacho kinatembea kwenye maji, kiwa kipimo cha kifaa kitakuwa kinafunika ukubwa huo huo wa maji lakini ikiwa uzito wa chombo utakuwa kidogo zaidi kuliko msongano wa maji chini ya ukubwa huo basi hakitazama. Ikiwa chombo kitakuwa na uzito kama wa ubao uliolowa kitazama. Unatengeneza meli nchi kavu kwenye warsha kisha unaipeleka kwenye maji. Kuweka meli hii ndani ya maji ni Tawakkul maana yake ni kuiwasilisha meli kwenye maji na maji lazima yaipokee . meli imetengenezwa na wewe unatakiwa kuiendesha na kituo cha mwisho ni chako. Unatakiwa kuwa na ujuzi juu ya kanuni za utengenezaji wa meli na kanuni za maji pia. Kama utaitengeneza meli kwa mujibu wa kanuni basi hutaiendesha jangwani bali utatakiwa kuiweka kwenye maji. Maji yana mfumo kutoka kwa Allah na umeingiza meli ambayo umeitengeneza kwa kuzingatia kanuni na kuiweka kwenye maji. Umekabidhi kanuni za meli kwenye kanuni za maji na yanaipeleka mbele. Allah ametengeneza mfumo na tumetakiwa kuzifahamu kanuni hizi na kufaidika nazo. Tumetengeneza meli na kuiweka kwenye maji na itaendelea kwenda juu ya maji madamu kanuni zitabakia salama.

Allah amemuumba mwanadamu, kaanzisha sheria, majukumu ya mwanadamu na kumfundisha. Na hakusema kwamba sasa nimekukabidhi ulimwengu huu na wewe ndiye mmiliki. Wewe ni mwanadamu ambaye una mipaka ambayo ndani yake una mamlaka na kwa mujibu wa hayo unafanya mambo hayo. Chochote unachokifanya katika jamii kinakuwa ni kwa mujibu wa kanuni za ulimwengu. Ulimwengu ni maji na jamii ni meli. Unapaswa kutengeneza jamii, kuiongoza, uchumi lakini unatakiwa kufahamu kwamba haki nilizopewa kwa ajili ya kufanya kila kitu inatakiwa ziwe katika wigo wa mfumo mdogo. Sasa umetengeza mfumo na kusema kwamba nitafanya kila kitu mwenyewe sio sahihi. Unatakiwa kufanya kila kitu kwa mujibu wa mfumo uliowekwa kwa ajili yako na kisha kuwasilisha katika mfumo wa Allah. Kama utakuwa umetengeneza meli kwa kuzingatia kanuni na kuiweka majini haitazama kamwe. Lakini kama utapuuzia kanuni za Allah na kisha ukawasili kwa Allah basi zitazama.

Wasomi wa maadili wamesema kwamba unapokuwa dhaifu katika kutenda mambo basi yakabidhi kwa Allah. Kama umekuwa dhaifu basi hukufanya sehemu yako. Unatakiwa kufanya sehemu yako, hiyo ni kama kujitengenezea meli mwenyewe. Unatakiwa kutengeneza mfumo kwa sababu hilo umepewa wewe. Mwenye nguvu na dhaifu wote hawa wanatakiwa kumtegemea Allah lakini wanatakiwa kufanya nafasi yao kwanza kisha kutegemea mfumo wa Allah kukabidhi sunna za Allah na hiyo ndio yenye kudumu kwa muda mrefu. Mambo yote ambayo hufanyika kwa kumtegemea Allah hubakia milele. Kama utafanya kitu kwa kupuuzia sheria za Allah na kisha ukakikabidhi kwa Allah kitazama, jamii zitaharibiwa. Unatakiwa kutengeneza meli mwenyewe kwa mujibu wa kanuni na sheria za Allah na kisha ukabidhi kwa Allah na kisha Allah atazifanya zifikie hatima. Hii ndio maana ya ki Qur’an ya Tawakkul.
Kama anavyosema Allah katika surah Maida, kwamba unapokuwa na Tawakkul basi Allah ataizuilia mikono ya maadui zenu, unatakiwa kuwa na Taqwa kwanza, ina maana kwamba tengeneza mfumo wako wa ulinzi kisha kabidhi kwa Allah. Kama utaishi maisha yako kama inavyo takiwa na sheria za kimungu zinazo kufanya kupata ulinzi basi kabidhi kwa Allah. Itafikia lengo lake.

Hotuba ya 2

Ikiwa mwanadamu utakuwa na Tawakkul basi Allah ataikata mikono ya maadui inayonyooshwa kukuelekeeni. Leo hii mikono yote inawatafuta waumini na wanataka kuangamiza kizazi . kwanza ni Gaza, kisha Keshmir, India, Yemen na ardhi zote za Waislamu zimezingirwa na mikono hii haijakatwa kama ilivyo katika ahadi ya Allah. Hii ni kwa sababu Allah alisema kwamba mnapaswa kupata Taqwa maana yake fanyia kazi mikakati yote ya kimungu kisha fanya mambo yale na kukabidhi kwa Allah. Tengeneza majeshi yenu, risasi na vikosi kisha kabidhi kwa Allah ambapo baada ya hapo Allah hataruhusu adui kukufikia. Kundi moja ndani ya Qur’an na

Pindi Allah anapo tuamuru kuwa na Taqwa na Tawakkul. Allah ameiweka kanuni hii na kisha kanuni ya Qur’an nikukusanya kila kinacho wezekana katika uwezo wako, kusanya farasi wako wa mafunzo, vifaru vya vita, na ufike mbele yako kisha mkabidhi Allah kisha hakuna mikono itakayo kufikia . ikiwa utakaa ndani na kufikiri kwamba Allah atakusaidia na kukulinda kinyume na kanuni za Allah. Wale ambao hawatekelezi wajibu wao, na kufanyia kazi majukumu yao kisha kinyume chake hutokea kwamba Allah hukukabidhi kwa maadui. Kundi moja katika Qur’an pia amesema Amirul Mu’minina (a) wasiopenda zaidi ni wale ambao Allah amewakabidhi kwa nafsi zao wenyewe, wanaweza kufanya chochote watakacho. Kuna ambao hufanya madhambi na hakuna kinachotokea. Kuna kundi jingine ambalo humuacha Allah na kuwategemea watu na hawa Allah huwakabidhi kwa watu na kuwanyang’anya kumkimbilia na wilayat. Na Allah hamuongozi mtu huyu. Na kuna watu ambao Allah huwakabidhi kwa mataghuti, madhalimu na watawala haya yapo kwenye hadithi kutokana na uhalifu wao. Madhalimu wanapaswa kuwaonea huruma . kuna baadhi ambao wana Tawakkal kwa Allah wanatekeleza majukumu yao kisha wanakabidhi kwa Waislamu.

Leo hii mikono ya maadui imeshawafikia Waislamu na Waislamu wamefedheshwa. Ni nchi moja tu ambayo imeonyesha ujasiri. Na hii ndio kanuni ya Allah kwamba sio kila aliyekuwa chini, na kufedheshwa na mtu mchafu kwamba atapambana na Allah na kuna kizazi kimoja tu cha Ibrahim ambacho kitasimama dhidi ya maadui na wengine wote waliosalia wanakwenda kwenye fedheha. Hili liliamuliwa hapo kabla kwamba popote ambapo fitina ya Wayahudi itakapoinua vicha vyao, kizazi cha Ibrahimu kitasimama. Leo kuna nchi 58 ambazo kuna magaidi, ISIS, Taliban, Al-Qaida na kuna makundi mengi ya wapiganaji na kati yao kuna kundi kubwa lipo pamoja na Pakistan lakini Allah hakuweka katika hatima yao kwamba mkono yao itaibuka kwa ajili ya kuwalinda Waislamu. Wakati wowote wanapopaswa kuua basi huwaua Waislamu tu. Mmoja katika makamanda wa ISIS alisema katika mahojiano yake kwamba tutapigana jihadi dhidi ya Wayahudi pale tu watakapokuwa mashia. Fikira hii ya watu w3a ISIS ipo kwa watawala wa Waislamu, wasomi na watu. Nchi ambayo Allah ameipa neema kubwa ya mfumo wa Wilayat. Leo hii watu wanapaswa kuona thamani ya mfumo wa Wilayat na kisha aweze kutofautisha baina yake na wale wanaofuata ukhalifa wa kidemokrasia wa samari hawawezi hata kuinua sauti zao. Lakini jamii ambayo ipo kwenye muhimili wa Wilayat imelifanya hili na imefanya tukio la kihistoria mbele ya maadui. Walifanya shambulizi ambalo hata maadui wenyewe walikiri kwamba tangia wazaliwe hawakuwahi kupigwa. Waarabu walipigana na Israil kabla a mwishowe walikabidhi nchi zao kwa Israel. Majirani wote wa Israel wanaishi maisha ya fedheha. Allah amewaandikia watu wa Wilayat kwamba Khaybar itaondolewa na Haidar na leo ni kupitia mtoto wa Haidar. Kwamba kijana amekuja nje yupo kwenye uwanja . hata hivyo baadhi ya habari za kulipiza kisasi zimekuja kutoka Israel ambapo watu walisikia milipuko. Hii ni vita ambayo siku zote huwa na pande mbili. Iran ilisema tulikuwa hatulipizi kisasi hadi leo kwa sababu maalumu na mikakati, lakini wakati huo umeisha na kwa sasa watajibu kwa nguvu kubwa hata kama utafanya kosa dogo. Hawaelezei nguvu yao kwa kushambulia kwa ndege zisizokuwa na rubani 300 na makombora na kutokea mipakani mwa Syria na Lebanon. Kufanya jambo hili kutokea Iran ambapo makombora na ndege zisizokuwa na rubani zilitua ndani ya Ardhi ya Israel na kwa kishindo ambapo walishindwa hata kupata muda w kutuliza. Hii ilikuwa n kuwaelezea kwamba mnakosea bado kuhusu kufahamu nguvu yetu. Mlikuwa mnadhani kwamba vikwazo vimetudhoofisha na badala yake vimetupa nguvu zaidi. Hili lilishuhudiwa na kila mtu ulimwenguni na nyoyo za Waislamu na wasiokuwa Waislamu zilifurahi. Sherehe zilifanyika Palestina kwamba baadhi ya nchi za Kiislamu zimetoa majibu lakini wengine bado wamekaa wakiinamisha vichwa chini kwa fedheha bila ya kuchukuliwa hatua yeyote.

Kwa namna matangazo yalivyokuwa yametolewa lakini ndani ya vita sera zilibadilika. Kwa mujibu wa taarifa za habari tarehe 22 Aprili Rais wa Iran Raisi anaitembelea Pakistan baada ya kuipiga Israel na kufurahisha nyoyo za Waislamu. Rais wa nchi wa taifa pambanaji anaitembelea Pakistan kitu ambacho kimefanya nyoyo za Wapakistan kupata furaha. Tunaomba kwamba safari hii iwe na usalama. Serikali ya Pakistan inapaswa kuwapa watu wa Pakistan nafasi ya kuelezea hisia za nyoyo zao kwa watu ambapo wameingiza furaha kwenye nyoyo za Waislamu. Masunni kwa mashia inabidi wapewe nafasi ya kuikaribisha shakhsia hii kubwa na kumruhusu kuzungumza na umma. Tuna habari kwamba hawataliruhusu hili. Hii ni fedheha kubwa. Inabidi mtoa fursa kwa sababu heshima yenu haitashuka na ni kwa sababu hamna heshima yeyote ambayo inaweza kupungua. Waache Waislamu wa Pakistan waelezee hisia zao kwa shujaa wao na toeni fursa ya kuwapa ushirikiano wenye kudhulumiwa. Nakumbuka kipindi kiongozi alipokuja kutoka Iran wakati wa Zia ul Haqq alipewa mapokezi ya kihistoria. Nina uhakika kwamba lau kama watu watapewa nafasi leo pia watu watafanya wenyewe. Ikiwa serikali haiwezi kufanya chochote kwa ajili ya Palestina basi wape watu fursa hii ya kufanya mapokezi makubwa na mazuri. Maadui wa Kizayuni watapata ujumbe kwamba nyinyi ni madhalili na uongozi wa Iran ndio wenye kupendwa zaidi kwetu na Wapakistan wanasimama na heshima na sio na fedheha. Watu wetu hawaelekei kwenye fedheha hatuwezi kuwapa dhamana viongozi wetu na wasomi wetu ambao wanakubali udhalilishaji wa aina yeyote lakini watu wa Pakistan wanaweza kutoa maisha yao kwa ajili ya heshima. Watu wenye njaa ya madaraka viongozi wao ni Muawiya na Yazid lakini kiongozi wa watu wema ni Hussain bin Ali na watu wote wa Pakistan ni wafuasi wa Imam Hussain isipokuwa wale ISIS ambao wanapiga kelele kwenye vyombo vya habari na kujaribu kupotosha watu. Wageni hawa wanakuja na sisi tunawakaribisha kabla ya wakati wake na kuiomba serikali ya Pakistan kutupa fursa ya kuwakaribisha. Inabidi muiombe serikali na ikiwa serikali haitaweka vikwazo basi jiandaeni. Kama wangelitembelea Pakistan kabla ya kuishambulia Israel basi kusingekuwa na haja ya kufanya maandalizi ya kuwapokea kwani ingekuwa ni safari ya kidiplomasia tu. Lakini baada ya mafanikio waliyo yafanya na kisha kuamua kuja kuitembelea Pakistan, basi ni wajibu wetu kutoa heshima kubwa kwa mtu huyu mheshimiwa. Tunafahamu kwamba kuna vitisho vingi vya kiusalama na Wairan hawapo kwenye amani sehemu yeyote. Hivyo uangalizi wa usalama upo mahala pake lakini serikali inaweza kupanga ulinzi na kisha kuwapa raia fursa ya kuelezea hisia zao. Hili litanyanyua ya Pakistan na itafidia upungufu uliopo kuielekea Palestina. Watu pia wanatakiwa kuandaa mapokezi mazuri na kutuma ujumbe kwa Amerika na Wazayuni kwamba upazaji sauti kwa ajili ya Palestina sio tu ndani ya Pakistan bali ni katika ulimwengu mzima isipokuwa mafisadi ndio wanao waongoza Waislamu ambao hawawaruhusu kupaza sauti zao. Huu ndio wakati ambao Allah atamlinda kila mtu.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *