Wizara ya Habari ya Somalia imetangaza mapema leo kuwa kuwa magaidi 97 wa al-Shabaab wameuawa wakati wa operesheni mbili ziilizotekelezwa na jeshi la nchi hiyo na vikosi vya usalama katika mikoa ya Galguduud na Shabelle ya Chini.
Kwa mujibu wa shirika rasmi la habari la Somalia (SUNA), Wizara ya Habari imeelzea katika taarifa kwamba magaidi 50 wa al-Shabaab waliuliwa na jeshi la nchi hiyo kwa ushirikiano wa vikosi vya wanamapambano wa kiraia katika eneo la Eil Ghoruf lililoko katika mkoa wa Galguduud.
Kwa mujibu wa SUNA, magaidi wengine 47 wa al-Shabaab waliangamizwa katika operesheni nyingine iliyotekelezwa na vikosi vya usalama katika eneo Gishan mkoani Shabelle ya Chini.
Hivi karibuni wanamgambo 21 wa kundi la kigaidi la Al-Shabaab waliuawa katika operesheni ya vikosi vya Somalia katika mkoa huohuo wa Shabelle ya Chini.
Al-Shabaab ni kundi la kigaidi la wabeba silaha lenye mafungamano na mtandao wa kigaidi wa Al-Qaeda na limehusika na operesheni nyingi za kigaidi ambazo zimeua mamia ya watu barani Afrika.
Wanamgambo wa kundi hilo la kigaidi wameshambulia mara kwa mara wanajeshi wa serikali na vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Afrika huko Mogadishu, mji mkuu wa Somalia, na wamefanya operesheni kadhaa za umwagaji damu katika maeneo mengine ya Afrika.