Magaidi washambulia kituo cha kijeshi katika mpaka wa Niger

Wizara ya Ulinzi ya Niger imetangaza kuwa, kundi moja la kigaidi limekishambulia kituo cha jeshi la Niger karibu na mpaka wa nchi hiyo na Chad.

Mashambulizi ya kigaidi yaliyoigubika Nigeria tangu mwezi Mei mwaka 2013 hadi sasa yamepelekea maelfu ya watu kuwa wakimbizi, kuibua njaa, kuongezeka umaskini n.k.  Mashambulizi ya awali ya kigaidi yaliikumba Nigeri mwezi Mei mwaka 2013; ambapo milipuko miwili ya mabomu ilitokea katika kambi ya jeshi na katika machimbo ya madini katika eneo la Agadez kaskazini mwa nchi hiyo karibu na mipaka ya Algeria na Libya.

Tangu mwaka 2014 ambapo  kundi la kigaidi na kitakfiri la Boko haram lilitekeleza mashambulizi yake ya awali huko Difa hali ya usalama ya nchi hiyo katika maeneo ya kusini mashariki karibu na mpaka wa Nigeria imezidi kuwa mbaya. Aidha mwaka 2017 mikoa ya Tillaberi na Tahoua inayopakana na Mali pia imekumbwa na ukosefu wa usalama kutokana na mashambulizi yanayosadikiwa kutekelezwa na makundi ya kigaidi huko kaskazini mwa Mali.

Wizara ya Ulinzi wa Taifa ya Niger imetoa takwimu zinazoonyesha kuwa, raia karibu laki saba na wanajeshi laki tano wameuliwa nchini humo katika hujuma za kigaidi tangu mwaka 2013 hadi sasa. Wizara hiyo aidha jana Jumatano ilitangaza kuwa, wanajeshi 14 wa nchi hiyo wamejeruhiwa, na wengine 6 na magaidi 17 wameuawa katika hujuma iliyofanywa na magaidi 50  dhidi ya kituo cha kijeshi karibu na mpaka wa nchi hiyo na Chad.

 

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *