Magendo ya binadamu yameongezeka mara 26 katika mpaka hatari zaidi duniani

Wizara ya usalama wa ndani ya Marekani imetangaza kuwa, pato linalopatikana katika biashara haramu ya magendo ya binadamu inayofanywa kupitia mpaka wa pamoja wa nchi hiyo na Mexico, ambao ni mpaka hatari zaidi duniani, limeongezeka kutoka dola milioni 500 mwaka 2018 na kufikia dola bilioni 13 kwa sasa.

Tovuti ya gazeti la New York Times imeripoti leo kuwa, kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na wizara ya usalama wa ndani, mashirika yanayojihusisha na biashara haramu ya magendo ya binadamu yana timu za wataalamu katika masuala ya lojistiki, usafirishaji, usimamizi, wa nyumba za siri za maficho na masuala ya uhasibu; na kwamba pato la mashirika hayo limeongezeka kutoka dola milioni 500 katika mwaka 2018 na kufikia hivi sasa dola bilioni 13.

Kwa upande mwingine, na kulingana na uchunguzi uliofanywa karibuni na Umoja wa Mataifa, mpaka wa pamoja wa nchi kavu wa Marekani na Mexico, unajulikana kuwa ndio eneo hatari zaidi la mpaka duniani.

Kutokana na kuongezeka maombi ya watu wanaotaka kuingia kimagendo nchini Marekani, soko la wafanya magendo ya binadamu limestawi na takwimu za matukio ya halifu ulioratibiwa na taathira zake hasi za vifo vya watu zimeongezeka.

Ripoti zinasema, katika mwaka uliopita, watu zaidi ya 5,046 walikamatwa na kushtakiwa kwa tuhuma za kuhusika na magendo ya binadamu, wakati idadi hiyo katika mwaka 2014 ilikuwa ni watu 2,762.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *