Mahakama Kenya yatoa waranti wa kutiwa mbaroni Wazayuni wawili kwa kubaka watoto wadogo

Mahakama nchini Kenya imetoa waranti wa kutiwa mbaroni Wazayuni wawili kwa makosa ya kubaka watoto wadogo na vitendo vya uasherati huko Shanzu katika Kaunti ya Mombasa.

Wazayuni hao wanaojulikana kwa majina ya Koren Avraham na Ashush David walikimbia nchini Kenya kwa madai ya matibabu baada ya kupewa dhamana ya Shilingi laki mbili za Kenya na hadi hivi sasa wanakwepa kurudi Kenya kuendelea na kesi yao.

Walipandishwa kizimbani mwezi Juni mwaka jana. Wakati huo wakili wao, Joseph Kanyi alidai kuwa wateja wake ni wagonjwa na wanahitaji kwenda Israel kutibiwa. Jaji Mkuu, Yussuf Shikanda ambaye ndiye aliyesikiliza kwa mara ya kwanza kesi ya Wazayuni hao, ametoa amri wa kutiwa mbaroni na kurudishwa Kenya kwa nguvu Wazayuni hao kwa kupuuza amri ya mahakama.

Wazayuni hao wawili waliingia Kenya tarehe 19 Juni, 2021 kwa visa za utalii kumbe lengo lao ni kufanya ufisadi, ubakaji na uasherati. Serikali ya Kenya imesema kuwa, Wazayuni hao waliwarubuni wasichana wawili wadogo wa miaka 14 na 15 kwa kuwapa shilingi 14,000 na simu mbili za bei ghali za mkononi kabla ya kuwafungia kwenye nyumba moja huko Bumburi na kuanza kuwabaka.

Imesemwa mahakamani kwamba, Wazayuni hao walitumia vibaya umaskini wa wasichana hao na kuwaingiza katika masuala ya uasherati.

Wazayuni hao piwa wanakabiliwa na mashataka ya kuwadhalilisha kijinsia watoto wadogo na kuwashikashika maeneo mabaya watoto hao katika siku za tarehe 20 na 25 Juni, 2021.

Wazayuni hao wameshitakiwa pia kwa kuchochea uasherati baada ya kumpa kila msichana shilingi 7,000 za Kenya, simu za mkononi na kifaa cha kuhifadhia umeme (power bank) ili kuwarubuni kufanya vitendo vya uasherati.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *