Mahakama yaamuru mwili uliozikwa 2020 ufukuliwe

Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu  Mkazi Kivukoni (Kinondoni) jijini Dar es Salaam imeamuru mwili wa mwanamke aliyefia mahabusu katika kituo cha Polisi Mburahati wilayani Kinondoni, jijini Dar es  Salaam, mwaka 2020, Stella Moses ufukuliwe na ufanyiwe uchunguzi kujua chanzo cha kifo chake.

Mahama hiyo pia imeamuru matokeo ya uchunguzi huo yawasilishwe katika vyombo husika ili kama kuna watu waliohusika na kifo hicho wachukuliwe hatua za kisheria.

Uamuzi huo umetolewa leo Desemba 19, 2022 na Hakimu Mkazi Mkuu Franco Kiswaga, kufuatia maombi yaliyofunguliwa na wanafamilia wa marehemu.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *