Makabiliano makali kati ya majeshi ya Wananchi wa Yemen na muungano wa Saudia katika mkoa wa Shabwa

‘Wadi al-Nahr’sehemu ipatikanayo katika eneo la Bayhan magharibi mwa mkoa wa Shabwa wa Yemen leo hii imeshuhudia makabiliano makali kati ya vikosi vya jeshi na Kamati za Wananchi wa Yemen kwa upande mmoja, na washiriki wa UAE kwa uungaji mkono wa Jeshi la Wanahewa la Saudia wakiwa upande mwingine.

Mashambulizi ya anga ya muungano wa Saudia unaoshirikiana na UAE yalifanyika katika sehemu kubwa iliyopo katika eneo la Harib kusini mashariki mwa mkoa wa Ma’rib.

Wapiganaji wa muungano wa Saudia wameyalenga maeneo ya Harb, Al-Juba, Al-Abadiyah na Al-Wadi kusini na mashariki mwa mkoa wa Ma’rib kaskazini mashariki mwa Yemen mara 45 ndani ya masaa machache yaiyopita, likiwemo eneo la Al-Yatamah na Maeneo ya Al-Sha’af yanayopakana na mkoa wa Najran nchini Saudi Arabia.

Picha zilizosambazwa na kitengo cha vyombo vya habari vya jeshi la Yemen zinaonyesha kuwa jeshi na kamati ya wananchi zimesitisha kuendelea kwa vikosi vinavyoshirikiana na Rais wa Yemen aliyeondolewa madarakani Bw. Mansour Hadi, akiungwa mkono na wapiganaji wa muungano wa Saudia kwenye Al-Anin Front katika eneo la kusini la Jabal Abyssinian magharibi ya Taiz jimbo la kusini mwa Yemen.

Saudi Arabia pamoja na UAE na Bahrain wakisaidiwa na Marekani na utawala wa Kizayuni iliunda muungano tarehe 26 Aprili 2015 kwa ajili ya kuivamia Yemen na kujaribu kumleta Rais Abdrabbuh Mansur Hadi aliyejiuzulu na kukataa kurudi madarakani, ingawaje katika kipindi cha miaka saba iliyopita, licha ya mashambulizi ya pande zote na mzingiro wa nchi kavu, baharini na angani, Yemen haijafikia malengo yake yoyote.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *