Kituo cha Utafiti wa Mambo ya Kizayuni cha Faraan: Shughuli za kampuni za ulinzi za kibinafsi hazikuwa halali Katika miaka ya sabini ya karne iliyopita. Sababu ni kwamba makampuni haya na matawi yake hayakuwa chini ya sheria yoyote au sheria ya kimataifa kwa ujumla. Lakini baada ya Vita Baridi, mambo yalibadilika. Kwa maana nyengine, Umoja wa Mataifa ulianzisha mbinu mpya kwa taasisi hizi, na kwamba kulingana na mbinu hizo mashirika ya usalama ya kibinafsi yanaweza kufanya kazi kisheria na kwa uhuru.
Lakini sababu kuu ilikuwa ni mapenzi ya Marekani na Uzayuni wa kimataifa. Baada ya kumalizika kwa Vita Baridi na kukithiri kwa ukuaji wa mtu binafsi na kijamii wa watu kuhusiana na masuala mbalimbali ya kisiasa na kimataifa, Marekani isingeweza kuvamia hata nchi moja kwa urahisi kwa ajili ya maslahi yake ya kiuchumi na kikoloni. Na kwa upande mwingine, ikiwajibika na mawazo ya umma ya jumuiya yake na jumuiya ya ulimwengu.
Kwa hakika, makampuni haya yalikuwa bima nzuri kwa shughuli za kijeshi na za kijasusi za Marekani na Israel katika nchi mbalimbali. Kwa sababu pia walikuwa na athari kubwa katika kupunguza gharama za vita na kupanua utawala wa harakati za Kizayuni. Kampuni hizi za usalama hushirikiana na vyama vyao vya umma au vya kibinafsi ili kuhamisha uzoefu, vifaa vya kijeshi na mafunzo, mipaka ya usaidizi n.k. Bila ishara yoyote ya uwepo rasmi wa kijeshi wa Amerika na Israeli na kujihusisha kwao moja kwa moja katika maoni ya umma ya ulimwengu.
Hivyobasi, Marekani inaona ya kwamba ili kufikia malengo yake itahitaji upanuzi wa makampuni hayo ya ulinzi ambapo itakua ni kwa manufaa yake. Kwa mfano, sehemu ya shughuli za kampuni hizi ni kutoa huduma za usalama na kijasusi ambazo, pamoja na kulinda watu binafsi, wawekezaji na taasisi za serikali, huiba habari za kisiasa, za kiuchumi na za kijeshi za nchi zinazolengwa. Jambo la kushangaza ni kwamba wakuu wa taasisi hizi huwa ni maafisa wa ngazi za juu wa usalama wa kijeshi wa Marekani na Israel.
Matokeo yake ni kwamba, makampuni haya ya ulinzi binafsi mara nyingi hujihusisha katika migogoro ya kimataifa na migogoro mbalimbali ya usalama na kiserikali duniani kote, na kwa maana nyengine, mashirika hayo hupata maslahi yao kwa njia hii. Mfano mzuri wa hili unaweza kupatikana nchini Iraq ya baada ya Saddam, ambapo baadhi ya wanakandarasi 500 wa kiraia walikuwepo. Chanzo chake ilikuwa ni mkataba uliotiwa saini na makampuni 200 ya Marekani na serikali ya Iraq. Na chakufurahisha Zaidi ni kwamba sehemu ya kazi ya kampuni hizi ni kutoa ushauri na mafunzo ya usalama. Jambo muhimu ni kwamba makampuni hayo katika mashauriano yao yanaelekeza mwajiri anayetakiwa katika serikali za Marekani, Uingereza, Ufaransa na utawala wa Kizayuni pamoja na masuluhisho yao yaliyopendekezwa; Na hii ina maana ya kuongezeka kwa nguvu za Kizayuni.
PS:
1 – https://www.yjc.ir/fa/news/6503297
2- https://tn.ai/1751349