Makamu wa Rais wa Iran: Marekani na Ulaya hazina njia nyingine ghairi ya kukubali JCPOA

Makamu wa Rais wa Iran anayehusika na masuala ya uchumi amesema, vikwazo na mashinikizo ndiyo silaha ya mwisho kabisa ya Marekani na Ulaya na akaeleza kwamba katika hali ya sasa wao hawana njia nyingine isipokuwa kuyakubali mapatano ya nyuklia ya JCPOA.

Mohsen Rezaee aliyasema hayo hapo jana alipohutubia kabla ya Sala ya Ijumaa ya mjini Shiraz, makao makuu ya mkoa wa Fars kusini mwa Iran; na akaongezea kwa kusema: nchi nyingi duniani zinafanya juu chini ili kuwa na mahusiano na kibiashara na Iran wakati hata bado haujafikiwa mwafaka kuhusu makubaliano ya JCPOA.

Aidha, Rezaee amebainisha kuwa adui anajaribu kutumia kila njia ili kuitawala Iran pamoja na nchi zingine za eneo, ambazo zina idadi ya watu wapatao milioni 500, na ana kiwewe kwa kuiona Iran ni nchi yenye nguvu yenye misimamo huru.

Makamu wa Rais wa Iran anayehusika na masuala ya uchumi ameendelea kueleza kwamba biashara na upitishaji nchini bidhaa zinazoelekea nje ya nchi ni suala linalopewa umuhimu na serikali na akabainisha kuwa, mapato ya fedha za kigeni hivi sasa yameongezeka maradufu na kwamba licha ya kuendelea kuwepo vikwazo huku mapatano juu ya JCPOA yakiwa bado hayajafikiwa, uuzaji mafuta nje ya nchi na wa bidhaa zisizo za mafuta umeongezeka kwa kiwango kikubwa sana na nchi nyingi zinazikubali bidhaa za Iran.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *