Wataalamu wa masuala ya Mashariki ya Kati wanaamini kuwa, kuhuishwa uhusiano kati ya Iran na Saudi Arabia kumelifikisha eneo hili katika sura mpya ya kimataifa, ambayo imesababisha kudorora kwa mahesabu ya Washington na kufeli kwa mipango ya Wazayuni na Wamarekani.
Watafiti wa masuala ya kisiasa wanasema kuwa kwa kuunga mkono makubaliano kati ya Iran na Saudi Arabia, China imeonyesha kuwa imeingia katika hatua mpya katika kushughulikia kesi katika eneo hilo nyeti, kama ambavyo Kurejeshwa kwa uhusiano huo wa kidiplomasia kulikwamisha mipango ya Wazayuni na Marekani wa kuitenga Iran katika eneo na kuunda Jumuiya ya Kujihami ya Nchi za Kiarabu ya NATO, hivyobasi kusababisha taathira chanya katika masuala muhimu kwenye eneo hili.
Miongoni mwa kanuni na sera za Jamuhuri ya Kiisilamu ya Iran ni “kutoingilia masuala ya ndani ya nchi nyingine”. Kuhusiana na suala hilo, Tehran haitoingilia mazungumzo kati ya pande mbili za Yemen au Saudi Arabia , lakini katika mazungumzo hayo, Tehran-Riyadh zitazungumza kwa ajili ya kulenga kumaliza mgogoro kati ya Yemen na Saudia na vilevile kuunga mkono wito wa amani kati ya nchi hizo mbili.
Wamebainisha kuwa, makubaliano kati ya Iran na Saudi Arabia yalibatilisha nadharia ya Iran-phobia ambayo Washington ilijaribu kuikuza katika nchi za Kiarabu pamoja na utawala ghasibu wa Kizayuni.
Watafiti wa masuala ya kisiasa wanasema kuwa, kuhuishwa kwa uhusiano huo kulisababisha mshtuko mkubwa kwa utawala wa Kizayuni na Wamarekani na kupelekea kufifia kwa siasa za utawala huo ghasibu wa Kizayuni kama vile kueneza ubabe wake na kuendeleza kile kinachoitwa dini ya Ibrahim.