Makundi ya Palestina yatoa indhari: Gaza inanyemelewa na maafa ya kibinadamu

Harakati za Palestina za HAMAS na Jihadul-Islami zimetahadharisha kuwa eneo la Ukanda wa Gaza linakabiliwa na hali mbaya sana ya kibinadamu kutokana na mzingiro wa kinyama liliowekewa na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel.

Faraan: Makundi hayo ya muqawama ya Palestina yameeleza katika taarifa baada ya kikao chao cha pamoja kuwa, kuna uzembeaji na ucheleweshaji katika kuchukua hatua za lazima za kukomesha mzingiro iliowekewa Gaza na kuwawezesha watu wa eneo hilo wapumue, huku kukiwepo na uwezekano wa wakati wowote ule hali ya Gaza kuvurugika kikamilifu.

Hamas na Jihadul-Islami zimesisitiza kwa kusema: “kukomeshwa mzingiro uliowekwa na utawala wa Kizayuni ni haki ya taifa la Palestina na hatutaitolea gharama yoyote ya kisiasa; na tunatilia mkazo pia juu ya udharura wa kuwepo umoja wa kitaifa baina ya vyama na mirengo ya Palestina.”

Baada ya kuushambulia mtawalia na kwa miaka kadhaa Ukanda wa Gaza na kushindwa kufikia malengo uliyokusudia, sambamba na makundi ya Palestina kutosalimu amri mbele ya jinai zake, hatimaye utawala haramu wa Kizayuni wa Israel ulichukua hatua ya kuliwekea mzingiro eneo hilo.

Licha ya kukabiliwa na mashinikizo ya kimataifa, utawala wa Kizayuni ungali unaendeleza mzingiro dhidi ya Gaza sambamba na kuzuia kupelekwa misaada ya kibinadamu na bidhaa za chakula na dawa kwa watu wa eneo hilo…/

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *