Mamlaka ya Ndani ya Palestina: Matamshi ya karibuni ya Lapid ni sawa na kutoa kibali cha kuuliwa Wapalestina

Wizara ya Mambo ya Nje ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina imesisitiza kuwa utawala wa Kizayuni unabeba dhima ya kuwa masuuli wa jinai zinazofanywa kwa Wapalestina, kukiukwa haki za raia hao, ardhi na matukufu ya Palestina kwa hatua yake ya kuwaunga mkono kikamilifu wauaji, watenda jinai, na magaidi wake.

Wazayuni maghasibu kila siku huvamia na kushambulia maeneo mbalimbali ya Palestina, kuwauwa shahidi na kuwajeruhi raia wa Palestina sambamba na kuwatia nguvuni ilikufikia malengo yao ya kujitanua. Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni juzi Jumatano alitangaza kuwa, hataruhusu kuhukumiwa mwanajeshi yoyote wa Kizayuni.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina jana Alhamisi iliwasilisha taarifa na kubainisha kuwa, utawala wa Kizayuni unahusika kwa jinai zinazofanywa dhidi ya raia wa Wapalestina, kukiukwa haki za raia hao, ardhi na matukufu ya Palestina kwa hatua yake ya kuwaunga mkono kikamilifu wauaji,watenda jinai, na magaidi wake.

Taarifa hii ambayo ilitolewa ikiwa ni radiamali kwa matamashi ya Yair Lapid Waziri Mkuu wa muda wa utawala wa Kizayuni imefafanua kuwa, matamshi ya Lapid ambapo ameonekana akijifakharisha kwa jinai zinazotekelezwa na wanajeshi wa utawala huo dhidi ya Wapalestina yanasisitiza juu ya kuendelezwa jinai za Wazayuni dhidi ya raia wa Palestina.

Mamlaka ya Ndani ya Palestina imetahadharisha kuhusu upuuzaji wa jamii ya kimataifa na Umoja wa Mataifa kwa jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya raia wa Palestinana kusisitiza kuwa:kwa mujibu wa takwimu; jinai za kila uchao za utawala wa Kizayuni zimekuwa jambo la kawaida katiak maisha ya raia wa Palestina na hakunauwajibikaji wowote wa kisiasa mkabala wa jinai zote hizo.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *