Mapigano makali yaendelea kushuhudiwa baina ya jeshi la Ethiopia na TPLF

Mapigano makali yanaendelea kuripotiwa baina ya jeshi la Ethiopia na wapiganaji wa Harakati ya Ukombozi ya Watu wa Tigray (TPLF) katika maeneo ya magharibi katika mpaka na jimbo la Tigray la kaskazini mwa Ethiopia.

Faraan: Ripoti zinasema kuwa, mapigano hayo yameshadidi zaidi jana na juzi huku juhudi za kuupatia ufumbuzi mgogoro huo za kieneo na kimataifa zikiendelea.

Aidha mapigano katika jimbo la Tigray yanashadidi katika hali ambayo, indhari mbalimbali zimeendelea kutolewa kuhusiana na hali mbaya ya kibinadamu katika jimbo hilo.

Hivi karibuni Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa alitoa wito wa kuhitimishwa vita na mapigano kati ya serikali ya Ethiopia na wapiganaji wa Harakati ya Ukombozi ya Watu wa Tigray (TPLF) kaskazini mwa nchi hiyo.

Serikali ya Ethiopia ilitoa amri ya kushambuliwa eneo la Tigray lililo kaskazini mwa nchi baada ya kuwatuhumu wapiganaji wa Harakati ya Ukombozi wa Watu wa Tigray (TPLF) kuwa walishambulia jeshi la serikali katika eneo hilo. Vita hivyo vimeutia wasiwasi mkubwa Umoja wa Mataifa.

Vita vya kaskazini mwa Ethiopia vimepelekea watu karibu milioni mbili kuwa wakimbizi na kuwafanya wengine zaidi ya laki nne kukabiliwa na baa la njaa.

Juhudi zote za upatanishi ambazo zimekuwa zikifanywa na taasisi za kimataifa ukiwemo Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika AU zimepuuzwa na kukataliwa na pande zote mbili zinazoshiriki katika vita hivyo.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *