Afisa wa zamani wa vita vya kisaikolojia katika Jeshi la Marekani ametangaza kuwa serikali ya nchi hiyo ni mkandamizaji mkubwa zaidi wa wanawake duniani.
Scott Bennett, afisa wa zamani wa vita vya kisaikolojia katika Jeshi la Marekani, amesema katika mazungumzo yake na Press TV kwamba Umoja wa Mataifa unapaswa kuangalia Marekani iwapo kweli unataka kugundua matukio ya ajabu ya ukiukwaji wa haki za wanawake duniani.
Bennett amesema kuwa Marekani inawatumia wanawake kama nyenzo katika mapinduzi yake ya rangi na kuongeza kuwa: Huu ni mfano mwingine wa operesheni ya kutaka kubadilisha utawala ambayo Marekani, Israel na Wazayuni wanajaribu kuifanya kwa kutumia tuhuma zisizo na msingi, na wanawatumia vibaya wanawake kama medani na uwanja wa vita dhidi ya Iran.
Akisisitiza kwamba hatua hizo hazitazaa matunda, afisa huyo wa zamani wa vita vya kisaikolojia katika Jeshi la Marekani amesema: Umoja wa Mataifa unaweza kuibua mjadala huu na kujaribu kuifanya dunia itambue na kuona ukweli.
Scott Bennett amesisitiza kuwa, “kweli ni kwamba Marekani ndiyo mkandamizaji mkubwa wa wanawake duniani.”