Mashirika ya kimataifa yatiwa wasiwasi na mgogoro wa chakula barani Asia

Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) na taasisi nyingine za Umoja wa Mataifa zimeripoti kuwa, idadi kubwa ya wakazi wa bara Asia hawana chakula cha kutosha kufautai kuongezeka ukosefu wa usalama wa chakula uliosababishwa na kupanda kwa bei na kuongezeka umaskini katika jamii.

Russia na Ukraine zina nafasi athirifu na muhimu katika kudhamini mahitaji ya chakula cha kimkakati kama ngano, mahindi na mafuta ya kula. Baada ya kuanza vita kati ya Russia na Ukraine mwishoni mwa Fenruari mwaka jana, Ukraine ilipunguza sana uuzaji wa bidhaa za chakula kwa nchi nyingine duniani na hilo limesababisha kushuhudiwa mgogoro mkubwa wa chakula duniani sasa.

Shirika la FAO na taasisi nyingine za kimataifa za Umoja wa Mataifa zimesema katika taarifa yao ya pamoja kwamba: mwaka jana wa 2022 karibu watu milioni 500 yaani watu wanane kati ya kumi wanakabiliwa na uhaba wa chakula kusini mwa Asia.

Hii ni katika hali ambayo zaidi ya watu bilioni moja pia wanakabiliwa na ukosefu wa usalama wa chakula kutoka kiwango cha wastani na kufikia kiwango cha juu. Ripoti hiyo imeongeza kuwa, kwa upande wa kimataifa  ukosefu wa usalama wa chakula uliongezeka kwa zaidi ya asilimia 29 mwaka juzi wa 2021; ambapo  mwaka 2014 ukosefu huo ulikuwa wa asilimia 21.

Ripoti hii ni uchunguzi wa tano wa kila mwaka uliofanywa na mashirika ya (FAO), (UNICEF), Shirika la Afya Duniani (WHO) na Mpango wa Chakula Duniani (WFP) kuhusu usalama wa chakula na njaa.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *