Maneno ya Sayed Hassan Nasrullah, Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah nchini Lebanon, katika mahojiano na kituo cha televisheni cha Al-Alam siku ya Jumanne, mazungumzo yake yalikuwa mazuri mno kiasi kwamba wale wenye kutafuta ukweli kuhusu maendeleo ya Lebanon na eneo hilo watafaidika zaidi na matamshi hayo.
Wasikilizaji wa mahojiano ya “Sayed Hassan Nasrullah” na Mtandao wa Al-Alam wamepata majibu ya maswali yao; Kwa sababu alizungumzia masuala muhimu miongoni mwao tishio la utawala wa Kizayuni dhidi ya Iran alichokiita kuwa ni tishio la kupindukia na la kipuuzi; Kwa sababu utawala huu hauna uwezo wakutosha wa kuivamia Iran, na unajua kwamba Iran haina mzaha katika nyanja hii, bali utawala huo unaufahamu ukweli huu vizuri, vilevile aliyekua Rais wa Marekani, Bw. Trump pamoja na kichaa alichonacho na misimamo yake mikali anaufahamu vyema ukweli huu.
Ama Kuhusu vitisho vya Israel vya kutaka kuangamiza makombora ya Hizbullah, Sayed Hassan Nasrullah amesema kua lau Israel ingekua na uwezo wa kufanya hivyo haingesita katika utekelezaji wa jambo hilo. Alisema “Wakati utawala wa Kizayuni unaposema kwamba tunataka kuharibu makombora ya Hizbullah, basi unahitaji uingia kikamilifu katika vita … Je, wanawezaje kuangamiza makombora yenye uhakika wa kulenga sehemu na yenye kuruka yanayomilikiwa na Hizbullah?”.Israel haitoweza kufikia malengo yake kwa kupigana na Hizbullah.”Israel inaposema inataka kuharibu makombora ya Hezbollah, je, inafahamu idadi yake ni kiasi gani ?”
Jambo lakuzingatia n kuwa, Katibu Mkuu wa Hizbullah iliyopo Lebanon, alibainisha kuwa Hizbullah ina wapiganaji zaidi ya elfu mia moja na kwamba ikiwa wataazimia kufanya mashambulizi yoyote kwa nchini ya Lebanon, Waisraeli watapigwa na butwaa kutokana na maajabu watakayokumbana nay, ikiwa ni pamoja na kuanzishwa kwa mfumo wa ulinzi wa anga kwa ajili ya kuzuia ndege zisizo na rubani za Israel na hili litawapa viongozi wa Kizayuni na kuifanya hofu hiyo kuongezeka maradufu.
Katibu Mkuu wa Hizbullah ameashiria kuimarika kwa Imarati na Bahrain na utawala wa Kizayuni na hatari zake dhidi ya mhimili wa muqawama kwa kusema: “Nchi ambazo zimerejesha uhusiano wao na utawala huo [wa Kizayuni] zimemnufaisha adui wa Israel katika masuala ya vyombo vya habari na ya kiuchumi, Lakini katika nyanja ya kijeshi, hawatoweza kuipa serikali usaidizi wowote. “UAE imenunua silaha zenye thamani ya makumi ya mabilioni ya dola za kivita tangu kuanzishwa kwake, lakini katika makabiliano yake ya kwanza ya moja kwa moja na Ansarullah, ilipiga kelele.”
Vilevile alitoa ushauri na wito kwa UAE kuondoka Yemen akisema kuwa: “Suluhu ni rahisi sana. Ondoka kwenye vita na usijihusishe”. Wewe ulikiuka mipaka yangu nami nikajibu. Utakapo acha uchokozi wako nakurudi nyuma, nami sitokua na pingamizi lolote dhidi yako. Kitakachoihifadhi UAE nakuifanya ibaki salama, ni kurudi nyuma na kuondoka Yemen. Imarati haihitaji silaha zozote ili kujilinda.UAE imenunua makombora yenye thamani ya makumi ya mabilioni ya dola, vilevile wapiganaji, silaha na teknolojia ya kijeshi tangu kuanzishwa kwake, Lakini ghala hili la hifadhi halikuweza kuwapa ulinzi.
Kutumia mabilioni ya dola katika kununua vifaa zaidi hakutoipa nchi ulinzi.Badala yake, Imarati inapaswa kujifunza kutoka kwa kaka yake mkubwa, Saudi Arabia, na mshirika wake wa kimkakati, Israel. “Je, wao silaha ziliweza kuwalinda?”
Nasrallah pia alikwepa suala la uamuzi wa Saad al-Hariri, akilaumu kutokuwepo kwa al-Mustaqbal katika uchaguzi huo, akisema kuwa kutokuwepo kwa mkondo mkubwa kama vile al-Mustaqbal kutakuwa na athari kubwa katika uchaguzi wa Lebanon.