Mataifa matano ya Kanda ya Sahel yanafanya luteka ya kijeshi magharibi mwa Niger, ikiwa ni mara ya kwanza kwa shughuli ya aina hiyo kufanywa katika eneo linalokumbwa na machafuko ya makundi ya itikadi kali.
Eneo la Sahel limegubikwa kwa miaka mingi na waasi wenye mafungamano na makundi ya waasi. Wizara ya ulinzi ya Niger imesema mataifa matano ambayo ni Burkina Faso, Mali, Chad, Niger na Togo tangu Jumatatu wiki iliyopita yamekuwa yakifanya mazoezi makubwa ya kitaifa katika kituo maalum cha mafunzo ya kijeshi mjini Tillia.
Mazoezi hayo ni pamoja na mbinu za kivita na mipango inayolenga kuimarisha uhusiano kati ya jeshi na raia wa maeneo yanayokabiliwa na vita. Shughuli hiyo inayotarajiwa kukamilika Juni 3, inaashiria luteka ya kwanza ya kijeshi ya pamoja kati ya nchi hizo tano.
Tawala za kijeshi nchini Burkina Faso, Niger na Mali ziliwafukuza wanajeshi wa Ufaransa, mtawala wa zamani wa kikoloni na zinaigeukia Russia kwa msaada.
Makundi yenye silaha yenye mfungamano na mtandao wa kigaidi wa al Qaida na kundi la Daesh yamekuwa yakitekeleza mashambulizi na kuibua hali ya katika maeneo ya sahel Afrika; hujuma ambazo zimepelekea kuuliwa maelfu ya watu na kusababisha mamilioni ya wengine kuwa wakimbizi.
Hayo yanajiri katika hali ambayo, Shirika la Kimataifa la Msaada wa Kibinadamu la International Rescue Committee (IRC) hivi karibuni lilitangaza kuwa, idadi ya watu wanaotaabika kutokana na ukosefu “mkubwa” wa chakula kwenye mataifa matatu ya kanda ya Sahel imefikia milioni 7.5.