Mgogoro wa nishati barani Ulaya, EU yashindwa kudhamini mahitaji ya wananchi

Idara ya Mazingira ya Ulaya imetangaza kuwa, juhudi za nchi za bara hilo za kpunguza mahitaji ya nishati na kudhamini mahitaji ya wananchi wake hazitoshi na si za kudumu.

Miezi minne iliyopita, nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya zilifikia makubaliano ya kupunguza matumizi na mahitaji yao ya nishati kama sehemu ya juhudi zao za kukabiliana na madhara ya vita vya Ukraine na hatua ya nchi hizo ya kuiwekea vikwazo vikubwa Russia.

Nchi hizo za Ulaya zilikubaliana kupunguza mwatumizi ya gesi kwa asilimia 15 na ya umeme kwa asilimia 10 lakini ripoti ya kina iliyotolewa tarehe 14 Disemba 2022 inaonesha kuwa makubaliano hayo yamepuuzwa na hayakutekelezwa ila kwa kiwango kidogo sana.

Shirika la habri la IRNA limeripoti habari hiyo leo na kunukuu ripoti mpya ya mtandao unaoundwa na asasi za kiraia zijuikanazo kwa jina la Idara ya Mazingira ya Ulaya (EEB) ikionesha kuwa, thuluthi nzima ya nchi za Umoja wa Ulaya zimeshindwa kutekeleza ahadi zao.

Ripoti hiyo imeongeza kuwa, kati ya nchi 27 wanachama wa Umoja wa Ulaya, nchi nane hazikuchukua hatua hata ndogo za kutekeleza makubaiano hayo ya kupungua matumizi ya gesi na umeme. Ni nchi 12 tu ndizo zilizochukua hatua ya kupunguza matumizi yao ya nishati tena kwa kulazimishwa sana.

Nchi ambazo zinategemea mno gesi ya Russia kama Italia na Ujerumani zimechukua hatua kali za kupunguza matumizi ya gesi, lakini nchi kama Austria, Finland, Luxenbourg, Holland, Sweden na nchi za Ulaya Mashariki, zimepuuza utekelezaji wa makubaliano hayo.

Kiujumla yataendelea kuwa ni majigambo tu ya kwenye vyombo vya habari ya nchi za Ulaya kuwa zinaweza kuishi bila ya nishati ya Russia hususan gesi wakati si kweli.

Previous Post
Next Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *